Header Ads Widget

TANESCO KILIMANJARO YAJIVUNIA MIAKA 60 YA KUKIMBIZWA KWA MWENGE WA UHURU. ..

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


SHIRIKA la Umeme nchini Tanesco mkoa wa Kilimanjaro limesema kuwa katika kuadhimisha miaka 60 ya kukimbizwa kwa Mwenge wa Uhuru nchini wamejipanga kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwemo kuwafikia katika maeneo yao ya makazi kupitia kampeni maalum ya Mobile clinic. 



Hayo yalibainishwa na Afisa uhusiano wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaisha Mbita wakati wa zoezi la uwashaji wa Mwenge wa Uhuru lililofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 



Alisema kuwa, katika kuadhimisha miaka 60 ya kukimbizwa kwa Mwenge wa Uhuru shirika hilo linajivunia kwa utoaji huduma bora ya usambazaji wa umeme. 



Afisa Uhusiano huyo alisema kuwa, Tanesco mkoa wa Kilimanjaro imekuja na kauli mbiu ya 'Tanesco Kilimanjaro fahari ya mteja' lengo la kauli mbiu hiyo ni wananchi kujivunia shirika lao katika miaka 60 hii ya kukimbizwa kwa Mwenge wa Uhuru. 


Kwa upande wake, Afisa Rasilimali watu wa Tanesco Kilimanjaro, Braison Swai alisema kuwa, kwa sasa shirika hilo limejipanga kikamilifu kukahikisha wateja wote wanahudumiwa vyema na kuridhishwa na huduma watakayoipata. 



Swai alitumia pia nafasi hiyo kutoa wito kwa wateja kutafuta taarifa sahihi zinazohusu shirika hilo kupitia vyanzo sahihi vya taarifa ili kujua kila kinachoendelea kuhusu shirika hilo pamoja na kutoa taarifa za changamoto zinazowakabili katika sehemu sahihi ili ziweze kutatuliwa. 

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI