Header Ads Widget

SEMINA YA MATUMIZI SAHIHI YA WALL PUTTY YAWAFIKIA MAFUNDI , KAMPUNI YA KIBOKO PAINTS YAPONGEZWA

 



Afisa Masoko Mkuu wa Kampuni ya KIBOKO PAINTS Bwn. Erhard Mlyansi akiongea na kujibu maswali mbalimbali ya Mafundi wa Kariakoo na maeneo ya karibu ,  kuhusu bidhaa hii mpya ya KIBOKO WALL PUTTY , katika semina fupi iliyofanyika Kariakoo Jijini Dar Es Salaam, Aprili 27, 2024.




Baadhi ya Mafundi kutoka maeneo ya Kariakoo , Keko , na maeneo jirani katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hawa.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja nchini kwa uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k  KIBOKO Paints, Imetambulisha Bidhaa yake mpya sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu kwa baadhi ya Mafundi Rangi wanaoishi na kufanya kazi karibu na eneo la Kariakoo Jijini Dar EsSalaam.

Hayo yamebainishwa Leo , April 27, 2024 katika Semina iliyotolewa na Kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa Mafundi Rangi wa Kariakoo na maeneo jirani.

Akizungumza baada ya Semina , Bwn. Hamidu ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema 

Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam imeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu na Mbezi na hatimae Kariakoo . 

" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi "  amesema Bw. Hamidu


Juma Ramadhan na Samwel Ryimo  ni baadhi ya Mafundi waliozungumza na Mwandishi Wetu Baada ya Semina hiyo wameipongeza kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa kuileta sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu 

"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " wamesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS