Header Ads Widget

ACT WAZALENDO YATOA MSAADA KWA WAFUNGWA WANAWAKE KIGOMA

     MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO KIZA MAYEYE AKIZUNGUMZA

Na Fadhili Abdallah,Kigoma
 
CHAMA cha ACT Wazalendo kimetoa msaada wa aina mbalimbali kwa wafungwa wanawake wanaotumikia kifungo kwenye gereza la Bangwe mjini ikiwemo kuwalipia faini wafungwa ambao walishindwa kulipa faini na kuanza kutumikia vifungo.
 
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma,Kiiza Mayeye akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo alisema kuwa utoaji huo wa misaada ni sehemu ya sherehe ya kuelekea maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama hicho ambayo kitaifa itafanyika mkoani Kigoma Mei mwaka huu.
 
Alitaja misaada ambayo chama hicho kimekabidhi kwa wafungwa wanawake ni Pamoja na taulo za kike, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupaka, miswaki,dawa za miswaki na nguo za ndani kwa wanawake sambamba na kuwalipia faini wanawake wawili waliokosa faini na kuanza kutumikia kifungo vituo vyote vikiwa na thamani ya Zaidi ya shilingi milioni moja.

    TATU AMANI MWENYEKITI WA NGOME YA WANAWAKE ACT WAZALENDO KIGOMA


Akizungumzia misaada hiyo Mwenyekiti wa ngome ya wanawake ACT wazalendo mkoa Kigoma,Tatu Amani alisema kuwa kutolewa kwa misaada hiyo kunatokana na namna walivyoguswa na hali za watu waliopo magerezani ambao wengine wamejikuta wako huko siyo kwa dhamira zao bali ni kutokana na yale yaliyotokea bila ridhaa zao.
 
Amani alisema kuwa wiki hii kuelekea maadhimisho ya siku ya ACT Wazalendo wameanza kutoa misaada gerezani lakini pia ipo ratiba ya kutembelea vituo vya Watoto yatima na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

VIONGOZI WA ACT WAZALENDO MKOA WA KIGOMA WAKIKABIDHI MISAADA HIYO
 
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wametoa taulo za kike kutokana na mahitaji kwa wanawake waliopo magerezani ili kuwafanya kuwa wasafi wakati wote kwani watu wengi wamekuwa wakisaidia misaada mingine na kusahau kutoa taulo za kike.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS