Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATAKA WANAFUNZI KUTOKA MAENEO YALIYOATHRIKA NA MAFURIKO WANAENDELEA NA MASOMO

 NA SCOLASTICA MSEWA, RUFIJI.



AAGIZA WANAFUNZI WAPOKELEWE SHULE JIRANI WAENDELEE NA MASOMO HATA KAMA HAWANA SARE NA MADAFTARI KWA SEHEMU ZOTE ZILIZOKUMBWA NA MAFURIKO NCHINI

 WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROF. ALDOF MKENDA AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Aldof Mkenda ametembelea baadhi ya shule zilizoathiriwa na mafuriko ya Mto Rufiji huko Kibiti na Rufiji na kuzungumza na Wanafunzi, Walimu na Wazazi na kuagiza Wanafunzi wote waliokuwa wakisoma katika Shule zilizoathirika na mafuriko nchini kwenda kuendelea na masomo katika Shule jirani zilizo katika maeneo salama ili waendelee na masomo yao.

Prof. Mkenda ametoa maagizo hayo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja Wilaya ya Rufiji na Kibiti kukagua shule zilizoathirika na mafuriko, kutembelea makambi pamoja na kutoa vitabu na madaftari kwa wanafunzi waliokumbwa na mafuriko  katika shule ya msingi Muhoro, shule ya Sekondari Muhoro huku akiangalia athari zilizosababishwa na mafuriko hayo.


Prof. Mkenda ametoa maagizo kwa Wazazi na walezi ambao wamekumbwa na mafuriko katika maeneo mbalimbali hapa nchini kuhakikisha watoto wao wanasoma shule zilizokaribu na maeneo waliyohamia.

Aidha amewaelekeza walimu kuwapokea wanafunzi waliotoka maeneo ya mafuriko bila masharti na kutoa taarifa kwa Maafisa elimu Ili kupata idadi kamili ya waliorudi shuleni.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi waliokuwa kwenye maeneo ya mafuriko wanaendelea na masomo popote walipo wakati taratibu nyingine zikiendelea za kuboresha miundombinu maeneo ambayo hayana mafuriko

"Mwanafunzi akija kwenye shule yako mpokee mengine yatatatuliwa baadae haya ni maelekezo Walimu wote wayasikie, Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza tuongezee nguvu kuhakikisha wanafunzi kwenye maeneo yaliyoathiriwa wanaendelea na masomo," amesema.

Prof. Mkenda alimuelekeza Katibu Mkuu wake kufanya tathimini ya miundombinu haraka na kuangalia namna sahihi ambayo itawasaidia Wanafunzi ili waendelee na masomo yao katika Shule ya Sekondari Muhoro kwa kuongeza miundombinu ya shule hiyo ili Wanafunzi hao wawe salama.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro. Carolyne Nombo amesema Wizara hiyo itahakikisha wanafunzi wote walipathirika na mafuriko wanaendelea na masomo bila kikwazo.

  MKUU WA MKOA WA PWANI ABUBAKAR KUNENGE 


Mkuu wa Mkoa wa PWANI Abubakar Kunenge amesema katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko watazungumza na wananchi na maamuzi ya Serikali yatafanyika kunusuru maisha yao kwa kuhamia sehemu salama..

Kunenge amesema baada ya mafuriko kipaumbele kiliwekwa kwa wanafunzi ambao wanatarajiwa kufanya mitihani mwaka huu na kutafutiwa shule kwa haraka na sasa wanafunzi wengine wanaendelea kurejesha shuleni kwenye maeneo ambayo wanaishi.

Afisa elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki ameeleza kwamba katika Wilaya ya Rufiji wanafunzi 7,264 wameathiriwa na mafuriko huku Wilaya ya Kibiti wanafunzi 824 wakikumbwa na adha hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI