
Dar es Salaam 9 Aprili 2024: TBL, moja ya watengenezaji wa bia na waajiri wakubwa nchini Tanzania na mshirika muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi, leo wamesaini Makubaliano na CRDB Bank Foundation ya kutekeleza kwa pamoja Mpango wa kufadhili mradi wa mbegu kwa wakulima wa shayiri.
Ushirikiano huu, unaotokana na mradi wa kilimo stahimilivu wa TBL, unawakilisha hatua muhimu katika juhudi za kampuni ya TBL za kukuza kilimo endelevu kitakacho wawezesha wakulima kote nchini.
Mpango huu wa Kilimo Bora (Smart Agriculture) wa TBL, una lengo la kuwawezesha wakulima wake moja kwa moja hadi asilimia 100% ifikapo mwaka 2025, Mkakati huu utahakikisha wakulima wanakuwa na ujuzi, ushirikiano na uwezo wa kifedha.

TBL inampango wa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji kwa kutumia rasilimali asilia hasa wakulima wa kilimo cha Mtama. Shayiri na zabibu.Ambazo ni rasilimali muhimu kwa shughuli za TBL, mpango huu unawasaidia wakulima moja kwa moja katika kuongeza uzalishaji na kutumia rasilimali asilia kwa ufanisi.
Kwa msisimko , Michelle Kilpin, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Breweries Limited, amesema: “Kwa kuunganisha juhudi za TBL na CRDB Bank Foundation, ushirikiano utasaidia kuongeza ukuaji wa sekta ya shayiri na kuimarisha ustawi wa kiuchumi wa wakulima wadogo wadogo nchini Tanzania.
0 Comments