Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa kwenye kambi ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji huko Wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akitoa taarifa ya hali ya athari za mafuriko katika Wilaya ya Kibiti kwa uongozi wa UWT taifa Mama Mary Chatanda wakati alipofika kutembelea na kuzungumza na waathirika wa mafuriko wa Wilaya za Kibiti na Rufiji Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Korombo..
Alisema Mwanamke aliyejifungua Kambi ya wahanga Mafuriko Mtomboli Kibiti ni Sabrina Khamisi Mwanzalima mwenye Umri wa miaka 19 Dini Muslim alijifungua tarehe 10/04/2024.
Kanali Korombo alisema watoto hao mapacha kwa mama huyo ni uzao wake wa kwanza. Wanaendelea vizuri wote wawili.
Aidha Mwenyekiti wa UWT taifa Mama Mary Chatanda alimpongeza mama huyo na akutoa viaa maalumu kwa mama huyo aliyejifungua watoto mapacha ikiwa ni pamoja blanket, baby show,kanga, vitenge na mabeseni ya kumwogeshea mtoto .
0 Comments