Header Ads Widget

BILIONI 38 KUJENGA CHUO KIKUU MUHAS KIGOMA

 

Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa  Appolinary Kamuhabwa (wa pili kulia) akikabidhi kwa  Mshauri Muelekezi kutoka  Kampuni ya OGM Consultant, Oswald Modu (wa pili kushoto) eneo ambalo kitajengwa   chuo cha MUHAS kampasi ya Kigoma
Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa  Appolinary Kamuhabwa (kulia) na  Mshauri Muelekezi kutoka  Kampuni ya OGM Consultant, Oswald Modu (kushoto) wakitiliana saini mkataba ambao MUHAS inakabidhi kwa mshauri elekezi kazi ya usimamizi wa mradi na eneo la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo cha MUHAS kampasi ya Kigoma
Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa  Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa  Chuo kikuu  MUHAS  kampasi ya Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHUO Kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kutumia  kiasi cha shilingi bilioni 38 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya chou hicho kampasi ya Kigoma ikiwa ni kutekeleza mpango wa serikali wa kuhakikisha wananchi wa mikoa yote ya Tanzania wanapata fursa za elimu ya juu.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Appolinary Kamuhabwa alisema hayo mkoani Kigoma  alitiliana Saini mkataba wa usimamizi wa mradi huo na  Mshauri Elekezi wa Kampuni ya OGM Consultant Bw. Oswald Modu utiaji Saini ulioshuhudiwa na Mkuu wa wilaya Kigoma,Salum Kali aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye.

Profesa Kamuhabwa alisema kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa jengo la utawala, jengo la maabara za kufundishia, kumbi za kutolea mihadhara (Lectures Theatre), mabweni ya wanafunzi na bwalo la chakula.

Akizungumza kabla ya utiaji Saini huo Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Profesa  Appolinary Kamuhabwa alisema kuwa  uanzishwaji wa Kampasi ya chou hicho mkoani Kigoma ni maamuzi ya serikali ya Jamhuri Tanzania katika kuhakikisha wananchi wa mikoa yote ya Tanzania wanapata fursa za elimu ya juu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kigoma, Salum Kali ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye kushuhudia utiaji Saini hati ya makabidhiano ya eneo la mradi alisema kuwa chou hicho kitakuwa mkombozi mkubwa kwa mkoa kuongeza idadi ya wataalam wa afya wenye taaluma ya elimu ya juu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS