Header Ads Widget

MCHAS YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI KUPITIA SEMINA MAALUM

 

Na Matukio Daima Media, Mbeya

Uongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Mbeya (MCHAS) umeandaa semina maalum ya siku moja kwa watumishi wake, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza tija, ufanisi na mabadiliko ya kifikra mahali pa kazi.


Semina hiyo imelenga kuimarisha weledi katika utumishi wa umma, uongozi, pamoja na kufungua fursa za ujasiriamali na uwekezaji ili kuwawezesha watumishi kujiandaa na maisha ya sasa na ya baadaye.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, alisisitiza umuhimu wa mtumishi kuwa tayari kujifunza kutoka kwa wengine na kupanua maarifa nje ya majukumu ya kila siku ya kitaaluma.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha MCHAS, Dkt. Geofrey Mdede, aliwashukuru watumishi kwa ushiriki wao na kueleza kuwa lengo ni kuwajengea uwezo mpana si tu katika utumishi wa umma na uongozi, bali pia katika masuala ya kiuchumi.

“Tunalenga kuwa na watumishi wenye uelewa mpana na wanaoweza kujitegemea kiuchumi kupitia ujasiriamali na uwekezaji,” alisema Dkt. Mdede.


Baadhi ya washiriki wa semina hiyo, akiwemo Evodius Emmanuel na Joyce Mponela, walieleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza uelewa katika masuala ya kiutumishi na kijamii, huku mada za uwekezaji na ujasiriamali zikionekana kuwa za wakati muafaka.

Semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa MCHAS wa kuhakikisha inakuwa na watumishi wenye motisha, uwezo wa kiuongozi na utulivu wa kiuchumi, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI