Header Ads Widget

MIAKA MITATU YA SAMIA PPRA YAJIVUNIA KUKAMILISHA VIPAUMBELE VYAKE

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma

KATIKA kipindi cha Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mamlaka Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imewezeshwa kutekeleza vipaumbele mbalimbali katika kusimamia ununuzi wa umma nchini, ambapo imeweza kutekeleza kwa mafanikio makubwa majukumu yake. 

Mamlaka imejikita katika maeneo makuu mbalimbali yakiwemo; Ujenzi wa  Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma, kuimarisha Ufuatiliaji na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, kuwajengea uwezo wadau wa Ununuzi wa Umma, kutungwa upya kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya Mwaka 2023, kujenga jengo la Ofisi ya Makao Makuu na kuanzishwa kwa Ofisi za Kanda.

Katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya uongozi wa awamu ya sita,  Serikali imetekeleza mambo mengi yanayoigusa sekta ya Ununuzi wa Umma ambayo yamekuwa na matokeo chanya kwa wadau wa sekta na kwa Watanzania kwa ujumla. 

UJENZI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UNUNUZI WA UMMA (NEST)

Amesema Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita (6) chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, umefanyika uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa Mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma unaojulikana kama National e-Procurement System of Tanzania (NeST). 

"Kabla ya uwekezaji huu, ununuzi wa umma ulikuwa ukifanyika kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma uliojulikana kama Tanzania National e-Procurement System (TANePS) ambao ulijengwa na kampuni ya kigeni kutoka Ugiriki. ," Amesema 

Na kuongeza " Serikali ilibaini changamoto nyingi kwenye ununuzi uliokuwa ukifanyika kupitia mfumo wa TANePS ikiwemo taarifa zote za Ununuzi wa umma kuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya kigeni nje ya nchi, " Amesema

Amesema Changamoto hiyo na nyinginezo zilipelekea uamuzi wa kuanzisha Mfumo mbadala ambao utakuwa bora zaidi, wenye kuleta tija, unaojengwa na wataalam wa ndani na kusimamiwa na Serikali.  

Amesema Chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ujenzi wa NeST ulianza rasmi Julai 2022 ambapo kufikia Julai 2023 ulianza kutumika rasmi. 

Ameeleza Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ilianzisha mfumo huu ili kuwezesha michakato yote ya ununuzi wa umma kufanyika kwa njia ya kielektroniki kwa lengo la kuongeza tija, ufanisi, uwajibikaji na uwazi  kwenye utekelezaji wa michakato hiyo. 

Amesema Mfumo wa NeST umeunganishwa na mifumo kumi na saba (17) ya Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi, kupunguza muda na gharama za michakato ya ununuzi, kudhibiti vitendo vya udanganyifu, rushwa na kuzuia ukosefu wa maadili. 

Aidha amesema zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali inatumika kwenye ununuzi wa umma, hivyo niwaase wananchi kujisajili katika mfumo NeST na kuomba zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Serikali ili kuweza kujipatia kazi na kinachotakiwa ni kuhakikisha anayeomba amekidhi vigezo vinavyotakiwa katika kuomba zabuni husika na pindi wanapopata zabuni wazifanye kwa uadilifu na ufanisi ili waendelee kuaminiwa katika miradi mingine.

Amebainisha kuwa zaidi ya Shilingi Trioni 29 imewekwa kwenye mfumo wa NeST kwa ajili ya kufanya ununuzi wa bidhaa, huduma na kazi za ujenzi, huku hadi kufikia Aprili 09, 2024 mikataba ya zaidi ya Shilingi Tilioni 5.14 imetolewa kwa wazabuni kupitia mfumo wa NeST, ambapo wazabuni 18,101 wamejisajili kwenye mfumo huo.

UWEZESHAJI MAKUNDI MAALUM KATIKA JAMII

Amesema Serikali ya awamu ya sita imewekeza katika kunyanyua wananchi wake kiuchumi kwa kuhakikisha inatoa fursa kwa Makundi Maalum wakiwemo vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu. 

"Ili kufikia lengo hilo, Mamlaka imewajengea uwezo Makundi Maalum na imekamilisha tafsiri ya miongozo miwili inayotumika katika ununuzi wa Umma, ambayo ni mwongozo wa ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa Umma na mwongozo wa ushirikishwaji wa jamii katika ununuzi wa Umma. ," Amesema 

Na kuongeza kuwa "Pia, imetafsiri  nyaraka sanifu tatu za zabuni za ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma, nyaraka sanifu moja ya zabuni za ushiriki wa jamii katika ununuzi wa umma.

amesema Kufuatia ushiriki wa makundi maalum katika ununuzi wa umma hadi kufikia Februari 2024, jumla ya tuzo za mikataba zenye thamani ya shilingi bilioni 1.95 zimetolewa kwa makundi maalum kupitia zabuni za umma zilizotangazwa na taasisi  nunuzi kupitia mfumo wa ununuzi wa kielektroniki (NeST), ambapo kundi la vijana wamepata tuzo za mikataba zenye thamani ya shilingi milioni 709 , wanawake shilingi bilioni 1.2 na wazee shilingi milioni 78.3.

KUONGEZEKA KWA KAGUZI NA UOKOAJI WA FEDHA ZA UMMA 

Mamlaka imekuwa ikifanya Kaguzi na uchunguzi mbalimbali na mapambano dhidi ya rushwa kwenye taasisi nunuzi. Lengo la kazi hii ni pamoja na kubaini kuwepo kwa ubadhirifu wa fedha za umma, matumizi mabaya ya madaraka na viashiria vya rushwa. Mara baada ya uchunguzi kukamilika, Mamlaka hutoa taarifa zake kwa taasisi nunuzi na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa.

Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita (6), Mamlaka ilifanya uchunguzi kwa zabuni zilizotekelezwa katika mwaka wa fedha 2021/22 na 2022/23, na kufanikiwa kuokoa jumla ya fedha za umma kiasi cha Shilingi Bilioni 16.27.

Kati ya fedha hizo,  kiasi cha Shilingi Bilioni 13.83 ilitokana na kuingilia kati kwa Mamlaka kwenye mikataba ambayo ilitolewa kwa wazabuni wenye bei ya juu wakati wenye bei ya chini wakitolewa kwenye mchakato (disqualified) na kiasi cha Shilingi Bilioni 2.44  ni kiasi kilichorudishwa na wasambazaji wa bidhaa (suppliers) na wakandarasi kwa malipo ya ziada yaliyofanywa na Taasisi Nunuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI