NA MATUKIO DAIMA, MAFINGA
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mtaalamu wa masuala ya uhandisi na miradi ya maendeleo, Mhandisi Modekai Michael Sanga, amechukua fomu kutia nia ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu mhandisi Modekai alisema kuwa ametia nia nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Mafinga mjini .
Mhandisi huyu aliyepata masomo katika Shule ya Msingi Wambi kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wavulana Iyunga jijini Mbeya elimu ya juu ya sekondari katika shule ya vipaji maalumu ya Ilboru mkoani Arusha, kisha kuendelea na Shahada ya Kwanza ya Uhandisi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (UCLAS), ambacho kwa sasa ni Ardhi University alisema anasifu kazi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya elimu nchini .
Modekai ni mhandisi aliyesajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania, mtaalamu mahiri wa usimamizi wa miradi mikubwa ya maendeleo, hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira alisema kuwa kaxi zinazofanywa ba serikali kwenye miradi maeneo mbali mbali ni kubwa sana.
Hata hivyo alisema wao kama wasomi wanaowajibu mkubwa wa kuendelea kueleza umma kazi nzuri zilizofanywa na serikali na kuepuka upotoshaji wa wapinzani juu ya kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na serikali ya CCM.
0 Comments