Header Ads Widget

MAFUNDI RANGI DAR ES SALAAM WAPEWA SEMINA .

 .

Baadhi ya Mafundi kutoka maeneo ya Mbezi , Goba , Malamba Mawili na Kinyerezi katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hawa , semina iliyofanyika Mbezi Mwisho Jijini Dar Es Salaam.



Mafundi wakiifanyia majaribio kwa kuipaka ukutani bidhaa ya KIBOKO WALL PUTTY , nje kidogo ya ukumbi ilipofanyika semina hiyo , Mbezi Jijini Dar Es Salaam.


Bwn. Amani Nduli kutoka kampuni ya KIBOKO PAINTS ( Kulia ) ambaye pia ni Mkufunzi wa Semina hiyo , akipokea maswali kutoka kwa mafundi waliohitaji kujua zaidi kuhusu bidhaa hii mpya ya KIBOKO WALL PUTTY.

Na Mwandishi Wetu.

Kampuni namba moja nchini kwa uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k  KIBOKO Paints, Imetangaza ujio wa Bidhaa yake mpya sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu tofauti na Bidhaa ya aina hiyo iliyopo sokoni kutoka Makampuni Mengine. 

Hayo yamebainishwa Leo , April 20, 2024 katika Semina iliyotolewa na Kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa Mafundi Rangi wa Ukanda wa Mbezi ambapo Mafundi kutoka GOBA , MALAMBA MAWILI , na KINYEREZI  wamehudhuria Semina hiyo . 

Akizungumza baada ya Semina , Bwn. Amani Nduli Mkufunzi wa Semina hiyo amesema 

Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam imeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu na Mbezi . 

" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi " 

Kwa upande wao Mafundi Rangi wameonesha kuifurahia KIBOKO WALL PUTTY baada ya kujaribisha kuipiga ukutani katika Semina hiyo , 

Ibrahim Dimoso , na  Emmanuel Kaoko ni baadhi ya Mafundi waliozungumza na Mwandishi Wetu Baada ya Semina hiyo wameipongeza kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa kuileta sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu 

" Tumeifanyia majaribio na ina Ubora zaidi kuliko wall putty nyingine tunazozitumiaga , KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni " wamesema.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS