SHIRIKA la Tanzania Health Promotion Support (THPS) limetoa misaada wa mahitaji mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko kwenye Wilaya za Rufiji na Kibiti.
Misaada hiyo ilikabidhiwa Mjini Kibaha na Mwenyekiti wa Bodi Profesa Mohamed Janabi ambaye amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na kushuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa (THPS) Dk Redempta Mbatia.
Prof Janabi amesema misaada hiyo ina thamani ya Shilingi milioni 18.8 milioni ni pamoja na vifaa vya
shule ni sare za shule, mabegi, madaftari na kalamu vyenye thamani ya shilingi milioni 7.8 huku kwa upande wa vyakula ni pamoja na unga wa mahindi kilo 1,500, maharage kilo 750 na mafuta ya kupikia dazeni 29.5 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni 10.9.
"THPS nao ni moja wapo ya wadau wakubwa wa afya wanaofanya kazi mkoani Pwani tumeungana na Serikali katika jitihada za kusaidia watu waliokumbwa na mafuriko,"amesema Prof Janabi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alitoa shukrani zake kwa THPS
kwa msaada huo na kusema kuwa anatarajia kuendelea kushirikiana na Shirika hilo na msaada huo utasaidia kuleta matumaini kwa watu waliopoteza mali na makazi kutokana na mafuriko hayo.
Mwisho.
0 Comments