Header Ads Widget

KISHINDO CHA SUGU UENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA NYASA, MUNGAI ,KIMBE NA MGONAKULIMA TOKA IRINGA WAONGOZA TEAM SUGU .

mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa William Mungai wa tatu kushoto akiwa kambi ya Sugu na makada wengine toka Iringa Suzana Mgonakulima mwenyekiti wa Bawacha na Alex Kimbe meya mstaafu wa Iringa 

Ni siku chache zimesalia kufungwa kwa zoezi ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa ambapo wanachama mbalimbali wameendelea kujitokeza katika ofisi za CHADEMA kuchukua na kurejesha fomu kwa ngazi mbalimbali.

TAZAMA VIDEO FULL HAPA BOFYA LINK HII

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Joseph Mbilinyi (Sugu) amerejesha fomu ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa na kupokelewa na Katibu wa CHADEMA kanda ya Nyasa Gwamaka Mbughi ofisini Kadege jijini Mbeya kwa niaba ya ofisi ya Katibu mkuu wa Chama hicho John Mnyika.


Akizungumza na wana-Chadema waliomsindikiza kwenda kurejesha fomu yake, Sugu amesema dhamira yake ni kwenda kuwaunganisha wanachama wa Nyasa kuwa wamoja na kutoruhusu makundi ya yoyote.



Amesema pamoja na mengineyo katika vipaumbele vyake kumi atahakikisha anasimamia ujenzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda ya Nyasa ambao amesema ataanza baada ya siku saba baada ya kuchaguliwa kwake kuongoza Kanda ya Nyasa.


Viongozi mbalimbali wa CHADEMA Kanda ya Nyasa wamemsindikiza Joseph Mbilinyi kurejesha fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Iringa William Mungai, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya Masaga Kaloli, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Mbozi, Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Iringa, aliyekuwa mgombea uenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Ahadi Mtweve na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa CHADEMA Mkoa wa Iringa Suzan Mgonukulima, amemtaka Sugu kujiamini na kwenda kufanya kazi kwa uadilifu akisema wafuasi wake wanaamini ana uwezo wa kuiongoza Kanda ya Nyasa na kwamba huu ni wakati wa mabadiliko.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya CHADEMA Digital Kanda ya Nyasa Pascal Haonga amesema anaamini Sugu akichaguliwa kuongoza Kanda hiyo atatimiza kiu ya kuwaunganisha wanachama na kupigania maslahi ya Taifa kupitia CHADEMA ambacho ni tumaini la wananchi.



Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa inaendelea kuwakumbusha wanachama kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwa ngazi ya Kanda sasa na kwamba zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu linaendelea na litafikia tamati Aprili 22, 2024 majira ya saa kumi Jioni.




Lengo la CHADEMA ni kusuka timu ya viongozi watakaowaongoza wanachama wa Chama hicho kwa miaka mingine mitano na kuendelea kukijenga Chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania bara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS