Fenesi au kwa jina la kisayansi (Artocarpus heterophyllus) ni tunda la kitropiki ambalo hukua Asia, Afrika na Amerika Kusini na linajulikana kuwa tunda kubwa zaidi linaloweza kuliwa ulimwenguni.
Mbegu na nyama ya tunda hili inaweza kuchemshwa na kuliwa katika kama kari; tunda likiiva kabisa linaweza kuliwa likiwa bichi na kutumika katika vyakula vitamu na vilivyo chachu.
Barani Afrika tunda hili huliwa mara nyingi likiwa limeiva lakini katika bara Asia linaliwa kama mbadala mzuri wa nyama katika matoleo ya mboga mboga ya mapishi ya asili kama vile nyama ya kuku.
Ingawa, badala ya nyama maarufu, fenesi haichangii kiwango sawa cha protini, kwa hivyo ni wazo zuri kuichanganya naviungo vingine vya protini kutoka kwa mimea kama vile maharagwe, kunde na njugu .
Shirika la Umoja wa mataifa FAO sasa limeorodhesha tunda hili la fenesi kama mojawapo ya mazao yaliyosahaulika barani Afrika ambayo yanaweza kusaidia kumaliza njaa na pia kupambana na aina mbali mbali ya maradhi .Hizi hapa baadhi ya faida za tunda hili
Kinga dhidi ya magonjwa
Fenesi ni chanzo muhimu cha aina mbalimbali za phytonutrients, misombo hii ya mimea ni kinga na inayoweza kusaidia kuzuia maendeleo ya baadhi ya magonjwa sugu, kama vile kisukari. Ina vitamini C, carotenoids pamoja na polyphenols na flavonoids.
Hutumika katika matibabu ya saratani ya tezi dume, saratani ya tumbo, saratani ya mapafu, magonjwa ya moyo na shinikizo la damu. Pia ina uwezo wa kuzuia mtu kuzeeka.
Chanzo cha vitamini na madini
Fenesi ina kiasi cha chini cha kalori wakati, kulingana na angalau utafiti mmoja ina virutubisho vingi zaidi kuliko matunda mengine mengi maarufu kama vile tufaha, parachichi na ndizi. Kwa kweli, mbegu na nyama yake ina kalsiamu na chuma zaidi kuliko matunda mengine ya kitropiki na ni chanzo muhimu cha vitamini B ikiwa ni pamoja na B1, B3, B6 na folate.
Inaweza kusaidia kuboresha afya ya moyo
Pamoja na kusambaza phytonutrients ya kinga fenesi pia ina virutubisho rafiki kwa moyo ikiwa ni pamoja na potasiamu na nyuzi.
Kuboresha kinga ya mwili
Ni viungo vya nyuzi katika tunda hili zinazosaidia utumbo pamoja na vitamini C na beta-carotene ambayo yanapendekeza kwamba fenesi inaweza kusaidia afya ya kinga na uwezekano wa kupunguza hatari ya kuambukizwa na virusi.
Mbali na hayo, kiungo kilichopatikana katika mbegu ya matunda kinaonekana kuamsha seli muhimu za kinga, zinazoitwa neutrophils. Seli hizi za kinga ni mojawapo ya mistari yetu ya kwanza ya ulinzi na huongeza nguvu za seli nyingine za kinga.
Kutengeza bidhaa nyingine
Kando na kutumika katika kuoka na kutengeneza sharubati na saladi. Fenesi inaweza kupikwa ikiwa kijani. Mbegu zinaweza kupikwa au kuliwa zikiwa mbichi.Pia fenesi hutengeneza Pipi, ice cream, juisi, mvinyo , jamu, na kachumbari.Majani yake hutumiwa kwa kawaida kulisha mbuzi na ni chanzo kizuri cha protini na nguvu.
0 Comments