Header Ads Widget

DKT BITEKO KUFUNGUA MKUTANO WA 13 WA TEF

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko anatarajia kufungua mkutano wa mwaka wa 13 wa kitaaluma utakaokutanisha Wahariri 150 kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana,Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Waharri Tanzania  (TEF) Neville  Meena amesema mkutano huo  utafanyika kwa siku mbili ambao utakuwa na mada mbalimbali.


“Tutakuwa na mkutano Mkuu wa 13 wa mwaka wakitaaluma utakaokutanisha Wahariri zaidi ya 150 kutoka katika vyombo mbalmbali vya habari ambao umebeba kauli mbiu isemayo  nafasi ya vyombo vya habari katika kuhamasisha matumizi ya gesi kwa ajili ya  kulinda misitu,”Amesema


Ameongza kuwa :”Mada zitakazo tolewa katika mkutano huo ni pamoja na nafasi ya wanawake katika vyombo vya habari, mada kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani na mabadiliko ya kiteknolojia katika vyombo vya habari,”


Katika hatua nyingine Meena amewataka waandishi wa habari kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha wananchi kutumia gesi ili kuendelea kulinda misitu.


Amesema ili kupunguza mabadiliko ya tabia ya nchi kila mwananchi anawajibu kuhakikisha analinda mazingira yanayozunguka eneo lake.


“Serikali inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanatoka katika matumizi ya kuni na mkaaa na kuenda katika matumizi ya gesi lengo ni kuhakikisha wanadhibiti hali ya uhalibifu wa mazingira,”amesema


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI