Header Ads Widget

TEF : WAANDISHI ZINGATIENI MAADILI NA MIIKO





Na Hamida Ramadhan, Matukio App Dodoma

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili na miiko ya kazi hasa katika kipindi hichi za kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu. 


Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mjumbe Kamati ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) Salim Said Salim alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wao wa kitaaluma wa 13 unaotarajiwa kufanyika Aprili 29 Dodoma. 


Amesema katika chaguzi zinazokuja waandishi wa habari watumike kama daraja la kuwavusha watu na sio kuwa kikwazo kwa kuchonganisha watu. 


" Tusiwe na ushabiki usiokuwa na tija na hivyo niwaombe waandishi wa habari kupitia uchaguzi huo twendeni tukaisaidie nchi na tuivushe salama katika kwenye chaguzi hizo zinazokuja, " Amesema Mjumbe huyo


Na kuongeza "Msije kujipa matumaini eti ya kwamba chaguzi zote zilizofanyika katika nchi yetu zilikuwa salama ukweli ni kwamba kulikuwepo na manun'guniko hivyo twendeni tukafanye kazi zetu kwa kuzingatia maadili miiko na Weledi wa kazi, "amesema 


Hata hivyo amewataka waandishi wa habari na wachamuzi wa habari za michezo futuata maadili na kuacha mihemko ambayo inapelekea watanazaji, wasilizaji na wasomaji kufahamu upande wa timu unayoshabikia. 


Pia amewataka waandishi wa habari kuwa nadhifu pale wanapofanya mahoniano na mdau bila kusahau heshima kwa mdau aliyekuzidi umri na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 


Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendani TEF Neville Meena amesema katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajuwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt, Doto Biteko huku mgeni wa heshima akiwa ni Waziri Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye. 


Aidha Mjumbe huyo amesema katika mkutano huo utaudhuriwa na jumla ya wahariri 150 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini akitaja ajenda zitakazojadiliwa nipamoja na: Uongozi wa wanawake katika vyumba via habari, Uchaguzi, Mabadiliko ya Teknolojia pamoja na Mabadiliko ya tabia nchi. 


Sambamba na hayo amewataka waandishi wa habari kuacha kunifungia na badala yake waniunge kwenye vyama vya kitaaluma ili kuweza kujulikana bila kusahau kupata fulsa za mafunzo zonazotolewa na vyama hivyo vya kitaaluma. 


Amesema kauli mbiu ya mkutano huo inasema "Nafasi ya vyombo vya habari kuhamasisha matumizi ya gesi kwa ajili ya kulinda misitu". 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI