NA WILLIUM PAUL, LUSHOTO.
MKUU wa wilaya ya Lushoto Japhari Kubecha Mghamba amefanya ziara ya kutatua kero za wananchi wa kata ya Shume, kijiji cha Hambalawei, ambapo alikutana na changamoto ya bei ya maji katika kijiji cha Hambalawei.
Kubecha amewaelekeza RUWASA bei ya maji ishuke kutoka Tsh.5000 mpaka kufikia Tsh.3,750 ambapo bei ya Serikali ya Vijijini ni kuanzia shilingi 1000 Mpaka 5,000/=.
Amewataka Wananchi wa kata ya Shume kijiji cha Hambalawei kuungana na kushikamana Kwa Maendeleo ya wanakijiji wa Hambalawei.
Mkuu huyo wa wilaya ameongeza pia kwa kusema Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan adhima yake ni kuondoa kero za Maji kwa Wananchi wake kuwa historia.
Mwisho....
0 Comments