Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Dubai tangu Jumatatu Aprili 15, 2024 zimesababisha uwanja wa ndege wa nchi hiyo kufurika maji.
Shirika la habari la Serikali ya Dubai (WAM) limeiita mvua hiyo kuwa ni "tukio la kihistoria la hali ya hewa" ambalo limezidi mvua zote zilizowahi kurekodiwa.
Pia, CNN imeripoti kuwa wastani wa mvua iliyonyesha kwa siku moja ni sawa na ya mwaka nzima katika nchi hiyo, iliyopo katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha lami ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai - uliotangazwa hivi karibuni kuwa uwanja wa ndege wa pili kwa shughuli nyingi zaidi duniani, umejaa maji mithili ya bwawa.
Hali hiyo imesababisha usumbufu wa shughuli za uwanja wa ndege huku mashirika mengi ya ndege yakiripoti kuchelewa kwa safari za ndege.
“Shirika la ndege la Flydubai liliahirisha safari zote za ndege hadi saa 4 asubuhi leo Jumatano,” imeripoti AP.
0 Comments