Header Ads Widget

CCM YATAKA WATANZANIA WAPUUZE MAANDAMANO YA CHADEMA NA WACHANGAMKIE MIKOPO YA 10%

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Katibu wa Siasa,Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makala amewataka wananchi kupuuza maandamano ya Chadema yaliyotangazwa kuanza April 22 mwaka huu kwa nchi nzima na badala yake wachangamkie Fursa za mikopo ya Asilimia 10 iliyorejeshwa na Serikali.


Mwenezi Makala ametoa kauli hiyo leo akiwa katika mkutano mkubwa wa CCM mjini Njombe wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM taifa mkoani Njombe ambapo amesema tayari Rais Samia ameruhusu kiasi cha shilingi bilioni 227 kitumike kwa mikopo iliyositishwa kwa vijana,Wanawake na wenye ulemavu hivyo muda wa kuandamana utumike kufuata mikopo hiyo.





Aidha Amesema Watanzania wanapaswa kupima kati ya Maandamano ya Chadema na Maendeleo kisha waamue kujiletea maendeleo ndani ya taifa lao kwani inasikitisha kuona Serikali inatangaza mikopo wakati wao wanatangaza Maandamano.


Awali mbunge wa jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika amesema Katika mkoa wa Njombe Serikali imefanya kazi kubwa ya kulipa fidia kwenye miradi mikubwa inayosubiriwa kwa hamu ya Chuma na makaa ya mawe wilayani Ludewa pamoja na kutenga kiasi cha shilingi bilioni 18 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kikuu cha Dodoma tawi la Njombe.


Naye Issa Ussi  Gavu katibu wa Oganaizesheni CCM Taifa ameonya tabia ya baadhi ya viongozi kutumia vibaya madaraka yao kujilimbikizia na kujipatia mali isivyo halali na kwamba huyo hafai kuwa kiongozi na atashughulikiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS