Dk.Eva Wakuganda Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo akizungumza wakati wa kliniki ya upimaji wa awali ya magonjwa ya moyo mkoani Kigoma
Baadhi ya wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza kwenye kliniki ya upimaji wa awali wa magonjwa ya moyo mkoani Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Watu 11,200 wamefanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo nchini ambapo asilimia 40 kati yao wamegunduliwa kuwa na tatizo la magonjwa hayo hivyo kuanzishiwa taratibu za matibabu.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk.Eva Wakuganda alisema hayo wakati wa kliniki ya siku tatu ya upimaji wa awali ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa mkoa Kigoma inayofanyika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni.
Dk.Wakuganda alisema kuwa katika upimaji huo uliofanyika asilimia 12 ya watu hao waligunduliwa kuwa changamoto kubwa ya magonjwa ya moyo hivyo kuhitaji huduma za dharula za matibabu hivyo kufanyiwa taratibu za kupata huduma Zaidi za kibingwa na kwamba changamoto kubwa ipo kwa watu kuchelewa kuanza upimaji na hivyo kuhita rufaa ya dharula kwa ajili ya kupata matibabu ya kibingwa.
Akizungumza wakati wa kambi hiyo ya upimaji wa magonjwa ya moyo Mratibu wa huduma za kitabibu katika hospitali ya mkoa Kigoma Mweni, Dkt. Boniface Kilangi ambaye alimwakilisha Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo alisema kuwa magonjwa ya moyo na shinikizo la damu kwa sasa yanashika nafasi ya pili kwa magonjwa yasiyoambukiza.
Dk.Kilangi alisema kuwa kliniki hiyo ya upimaji imelenga kuwafikia watu 300 kila siku hivyo wanategemea Zaidi ya watu 300 kupatiwa huduma za upimaji na hiyo itakuwa na msaada mkubwa kwao kwani elimu watakayopata itasaidia kuanza kufanya uchunguzi mapema kutokana na watu wengi wamekuwa wakifika hospitalini hapo wakiwa wamechelewa hivyo kuhitaji rufaa ya dharula kwa ajili ya kupata huduma za kibingwa.
0 Comments