Watu wawili
wamefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Tanangozi, mkoani Iringa,
baada ya kudondokewa na lori lililokuwa limebeba mbao likitokea wilayani Mufindi mkoani humo.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo, wamesema watu hao ambao ni mwanamke na mwanaume walikuwa
wakitokea msibani eneo ambalo lipo Jirani na ajali ilipotokea, hivyo walikuwa
wakisubiria usafiri pembezoni mwa barabara hiyo.
Jimson Sanga
ni rafiki wa marehemu, Isaack Mkocha, amesema, marehemu alikuwa anatokea kwenye
msiba, na wakati ajali hiyo inatokea alikuwa
akisubiria usafiri wa kurudi Iringa mjini, ambapo ndipo anaishi na familia yake.
Katika hatua
nyingine Sanga ambaye ni mkufunzi katika chuo kikuu cha Iringa, amesema licha
ya kuwa marehemu ni rafiki yake pia anafanyakazi na mke wa marehemu huyo, hivyo
chuo hicho kimepata msiba.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa mkoa wa Iringa, Daktari
Alfred Mwakalebela, amesema march 26, 2024 majira ya saa 8 mchana walipokea
miili ya watu wawili ambao ni mwanamke na mwanaume na miili yao ilikuwa na majeraha mbalimbali.
0 Comments