Header Ads Widget

SERIKALI KUYAENDELEZA MASHAMBA YA CHAI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma


SERIKALI imesema ikotayari kuchukua mashamba ya chai na kuyaendeleza lengo ikiwa ni kuweka Sawa sekta hiyo ili iweze kusonga mbele na hawatavifunga viwanda vya chai. 


Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa bodi ya chai . 


Kutokana na hilo Waziri Bashe amesema watakaa pamoja na wadau kujadili na kukubaliana ili kuona kuna changamoto gani zinazowakabili ili waweze kuzitatua na Viwanda visonge mbele.


Amesema kuna athari nyingi za kufunga Viwanda kwa watu mbalimbali ambayo wamewekeza hapo, ikiwemo kukosa wa ajira kwa baadhi ya watu


"Hatutakubali kufunga Viwanda,badala yake tutakaa chini na kujadiliana kuona tunafanya nini,"amesema Bashe.


Aidha amesema walipokea ombi la kufungwa Viwanda kutoka kwa MO Enteprises lakini hawajakibaliana nalo na badala yake watakaa chini kuzungumza na wadau hao.


"Tumekataa ombi la kufungwa kwa kiwanda cha Chai cha Mo Enteprises,pamojana viwanda vingine kwa sababu vitaleta athari kubwa kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda hivyo, "Amesema.


Na kuongeza kusema "Zipo changamoto ambazo serikali zinakutana nazo lakini wanaendelea kuzifanyia kazi ili ziweze kuondolewa, " Amesema Waziri Bashe


Amesema kama Wizara wanaendelea na vikao baina yao na wizara ya fedha ili kuona kile wanachohitaji kwa ajili ya sekta ya chai waweze kusaidia.


Amesema hakuna kitu kinachoshindika mbele ya serikali,tutajipanga kuhakikisha tunapiga hatua moja mbele kwenye sekta ya chai.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Chai Mary Kipeja amesema wakulima wadogo wa zao hilo wanadai sh Bilion 2.8 kwenye Viwanda Jambo ambalo linawarudisha nyuma.


Amesema fedha hizo ni nyingi sana,ambapo wameiomba serikali kusimamia hilo ili waweze kupata fedha zao.


"Wakulima wadogo wanadai fedha zao kutoka kwa Viwanda,naomba suala hilo lifanyiwe kazi ili wakulima wapate haki yao,"amesema Kipeja.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI