Header Ads Widget

WAKRISTO WATAKIWA KUENZI UPENDO WA YESU KRISTO

 




Na Matukio Daima APP , Kigoma.

Wito umetolewa kwa waamini wa kanisa katoriki kuuenzi upendo wa Bwana Yesu aliyekufa msalabani kwa ajili yao kwa kuwa kufa msalabani ni ishara ya upendo na ukombozi.


Wito huo umetolewa na Makamu Askofu jimbo katoriki Kigoma, Padre Evaristi Guzuye wakati wa hitimisho la maandamano ya  ibada ya  njia ya msalaba iliyofanyika kuanzia Parokia ya Mtakatifu Vicenti wa Paulo Katubuka hadi kituo cha Hija Buhabugali kilichopo eneo la katonga Mkoani Kigoma.


Padre Guzuye alisema, siku ya ijumaa kuu ni siku ambayo waamini wote wa kanisa katoriki duniani wanaadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha Bwana Yesu Kristu, kifo ambacho kinaambatana na mateso makali hivyo kutokana na ibada ya leo waamini wote wanaswa kutokata tamaa kwa kubeba mahangaiko ya wengine ikiwa ni kuuenzi upendo walioachiwa na Yesu.


"Siku ya leo tunaadhimisha ijumaa kuu, siku ya ijumaa kuu ni siku ambayo bwana wetu Yesu Kristu alikufa kifo cha juu ya msalaba kwa mateso makali mno, ni siku ambayo dunia nzima waamini wote wa kanisa katoriki tunakusanyika kwa ajili kukumbuka kifo hicho na ujumbe ambao wa leo ni kwamba kwa Kifo hiki kinatukumbusha kuwa Bwana Yesu alitupenda, na aliyatoa maisha yake kwa ajili yetu. Alisema Padre Guzuye.


Akizungumza katika maandano hayo ya njia ya msalaba Paroko msaidizi Parokia ya Bikira Maria  Mshindaji Kigoma Padri George  Ntomoka amesema lengo la kuandamana ni kutaka waamini wapate muda mrefu wa kusali huku wakiyatafakari mateso ya Bwana Yesu Kristu.


"Waamini wapate muda mrefu wa kuyatafakari mateso ya Bwana wetu Yesu kristu hali kadhalika sababu ya kuhitimisha katika kitu hiki cha hija cha Jimbo ni, maandano haya ni sehemu ya hija hivyo waamini wamepata fulsa ya kushiriki hija kwa ijumaa kuu hii ya mwaka 2024" Alieleza Padre Ntomoka


Kifo cha Bwana Yesu Kristo ndiyo kiini cha imani yetu, Yesu aliteswa akafa na akafufuka ambali ndilo fumbo la wokovu wetu, hivyo tunapaswa kujifunza kwamba kifo mateso yake anapaswa kuimalisha imani yetu kama Wakristo wa Katoriki.


Kwa niaba ya kamati ya maandalizi Katekista kigango cha Katubuka Scholastica John amesema wiki kuu ni wiki ambayo imebeba azimisho kubwa la siku 40 za mfungo wa kwaresma, wiki kuu imebeba hitimisho la kazi ya Yesu Msalamabani.


Kupitia wiki hii wakristu wote hasa wakatoriki wanapaswa kuyaishi maisha ya Bwana Yesu kwa kuuenzi ependo anaoufanya juu yetu na kuyaishi maagizo yaliyotolewa na Yesu kwa kutambua kazi aliyoifanya msalabani.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS