Header Ads Widget

WAKAZI KIBAHA WALILIA DALADALA KUPITA TUMBI


NA MATUKIO DAIMA APP 

WAKAZI wa Kata ya Maili Moja Wilayani Kibaha wamemlilia mkuu wa Wilaya kuwasaidia kuzitaka daladala kupita barabara ya Tumbi ili kupata huduma za kijamii.

Kero hiyo ilitolewa kwenye mkutano wa hadhara ambapo mkuu wa Wilaya aliwakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya Moses Magogwa, mkutano uliofanyika kwenye Mtaa wa Uyaoni wa kusikiliza kero na changamoto kwa wananchi wa Kata ya Maili Moja.


Moja ya wananchi wa mtaa huo Agatha Kapinga alisema kuwa barabara hiyo ya Tumbi ina umuhimu mkubwa lakini hakuna usafiri wa daladala kupita huko ambapo ni barabara ya zamani ya Morogoro.


Kapinga alisema kuwa Tumbi kuna huduma muhimu ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Tumbi, Shule kuanzia Chekechea hadi Sekondari, Maktaba, Vyuo vya Udktari na VETA, Msikiti na Makanisa na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) ambako kuna huduma mbalimbali za kijamii.



Alisema kuwa ili kufiia huko huwabidi kupanda pikipiki ambapo gharama yake ni shilingi 2,000 ambayo ni kubwa na kwa wasiyo na uwezo huwabidi kutembea kwa miguu.


Aliongeza kuwa hata daladala ambazo zinafanya safari ya Mbezi Bokomnemela zikifika Njuweni haziendelei na safari na kuwafanya abiria kupanda pikipiki kuendelea na safari.


"Endapo usafiri wa daladala utakuwepo utatusaidia kutupunguzia gharama kubwa ambazo tunatumia kwa sasa hichi ni kilio kikubwa kwetu tunaomba utusaidie,"alisema Kapinga.


Kwa upande wake Katibu Tawala huyo Moses Magogwa alisema kuwa ataongea na mamlaka husika ya Usafirishaji Ardhini (LATRA) Mkoa wa Pwani ili kutatua changamoto hiyo.


Ikumbukwe eneo la Tumbi kwenye Shirika la Elimu Kibaha ndiyo mji ulioanza wakati wa kuanzishwa Mkoa wa Pwani ambapo kuna Hospitali ya Tumbi, Shule ya Msingi Tumbi, Shule ya Kibaha Wavulana na WasichanaTumbi Sekondari, Chuo cha Veta na Chuo cha Udaktari.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI