Header Ads Widget

WADAU WAOMBA MABADILIKO YA SHERIA YA UDHALILISHAJI

 


WADAU wa kutetea  Haki za Wanawake na Watoto wameiomba Serikali kufanya marekebisho ya Sheria na kanuni ambazo ni kandamizi kufikia usawa wa kijinsia pamoja na mapambano dhidi ya vitendo vya Udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ambavyo vinakithiri visiwani Zanzibar.


Wito huo umetolewa na Mwenyekiti  wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Sabiha Filfil Thani katika hafla maalum ya Dua, Darsa na Iftari iliyoandaliwa na Taasisi ya The Worriors Women  na kufanyika Kariakoo Mjini Magharibi Unguja.


Amesema licha ya kuwepo kwa Sheria mpya bado kuna haja  ya kufanya mabadiliko ya Sheria  hiyo ili kufikia usawa wa kijinsia pamoja na mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.


Hata hivyo ameeleza kuwa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ipo tayari kupokea maoni  kwa Sheria na Kanuni ambazo zinapungufu na zinahitajika kufanyiwa maboresho ili kukabiliana na vitendo vya Udhalilishaji kwa Wanawake na watoto.


Mapema Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya The Worriors Women  Sabra Machono ameeleza kwamba, lengo kuu la kuandaa hafla ya Dua, Darsa na Iftari ni kuwakutanisha pamoja wanawake kutoka makundi mbalimbali na kujadili pamoja namna bora ya kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia sambamba na mbinu  za kuwainua Wanawake nchini.


Zaidi ya Wanawake 200 wameshirikia katika hafla hiyo ambayo hufanyika kila mwaka lengo likiwa kujadili change motor zinazowakabili wanawake kiuchumi ikiwemo Udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI