Na Hadija Omary
Viongozi wa vilabu vya mpira vilivyopo wilayani kilwa Mkoani Lindi wametakiwa kusajili timu zao ili kuvifanya kuwa halali na baadae kunufaika na fursa mbali mbali.
Wito huo umetolewa na afisa utamaduni wa Wilaya ya kilwa Zamarad Mlangi jana March 07/2024 alipokuwa anazungumza baada ya kumalizika kwa final za michuano ya mpira wa miguu za Songosongo Diwani cup 2023/2024 iliyowakutanisha timu ya mapanya fc dhidi ya swamida fc uliochezwa katika viwanja vya funguni stadiam huko Wilayani Kilwa.
Amesema zipo faida nyingi kwa vilabu kusajiri timu zao ikiwa pamoja na kucheza mashindano mbalimbali katika ngazi ya wilaya na Mkoa pamoja na kupata fursa ya mikopo itakayowezesha timu katika maswala mbalimbali kutoka katika taasisi za fedha
Hasan Swalehe ni duwani wa kata ya songosongo ameahidi kuendelea kusaport michuono hiyo ya Songosongo Diwani cup kwa msimu wa 2024/2023 ili kuendelea kuinua vipaji kwa vijana wa kata hiyo.
Hata hivyo ameishukuru kampuni ya kuchakata gesi asilia ya SONGAS kwa kuwezesha mashindano hayo katika vitu mbalimbali ikiwa pamoja na jezi na fedha taslimu .
Nao baadhi ya wachezaji wa timu hizo zote mbili wamempongeza diwani wao kwa kuanzisha michuono hiyo ambayo imekuwa ikiinua vipaji vya vijana wa kata hiyo.
Katika michuano hiyo ya Songosogo Diwani cup umemalizika kwa mikwaju ya penat ambapo timu ya swamada fc imeibuka kidedea kwa kushinda kwa goli tano kwa nne na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 1.2 na mshindi wa pili ambae ni Mapanya fc kujinyakulia kitita cha pesa Taslimu cha shilingi 740,000.
0 Comments