Header Ads Widget

HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI KUENDESHA VIKAO VYAKE KIDIGITALI.



NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

 

HALMASHAURI ya wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro imebadilisha teknolojia ya ushiriki wa vikao vya halmashauri hiyo kutoka kwenye mfumo wa makabrasha na kutumia vishikwambi kwa Madiwani na wakuu wa idara.

 


Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Shedrack Mhagama alipozungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa, kubadilika kwa mfumo huo utasaidia halmashauri hiyo kupunguza matumizi ya fedha ambayo yalikuwa yakitumika kuandaa makabrasha hayo.

 


“Tumekuwa tukitumia gharama kubwa kila wakati kwa kutengeneza makabrasha ambapo zipo taarifa nyingi za kuripoti kwa Madiwani hasa kwenye kikao cha robo mwaka lazima turipoti shughuli mbalimbali za halmashauri zilizofanyika kila baada ya miaka mitatu” alisema Mhagama.

 

Alisema kuwa, kamati ya fedha imekuwa ikifanya vikao vyake kila mwezi ambapo halmashauri hiyo imekuwa ikizalisha makabrasha kila wakati na kufanya matumizi kuwa makubwa.

 


Mhagama alisema kuwa, mbali na gharama za utengenezaji wa makabrasha hayo lakini pia halmashauri ilikuwa inaingia gharama za kusafirisha nyaraka hizo kuwafikishia madiwani wote 42 siku saba kabla ya kikao ili aweze kupitia.

 

Alisema kuwa, kupitia vishikwambi itaisaidia halmashauri kuwasiliana na Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara kupitia mtandao pamoja na taarifa za vikao kuwafikia kwa njia hiyo.

 


Mkurugenzi huyo alisema kuwa, teknolojia hiyo itasaidia kurahisisha utatuaji wa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kwani taarifa zitafika kwa wakati pia itasaidia kuhakikisha utunzaji wa siri za nyaraka za serikali.


Kwa upande wake, Afisa Tehama wa Halmashauri hiyo, Absalim Yese alisema kuwa, kuanza kwa mfumo huo wa kutumia vishikwambi itapelekea halmashauri hiyo kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika katika uandaaji wa nyaraka pamoja na kuzisambaza.

 


Yese alisema kuwa, mfumo utakaokuwa unatumika utakuwa unasimamiwa na mamlaka ya mtandao (IGA), ambapo utaratibu shughuli zote za vikao rasmi ndani ya serikali.

 

“Niwatoe wasiwasi Wananchi kuhusu usiri wa taarifa mfumo huu umezingatia usiri mkubwa ili kuhakikisha taarifa za halmashauri ya moshi haziendi nje na maeneo yasiyohitajika hivo uhakika wa kutunza taarifa za serikali kwa usiri ni mkubwa” alisema Yese.

 

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI