NA MATUKIO DAIMA MEDIA
VIJANA 140 toka familia zenye mazingira magumu kata za Mdabulo ,Ihanu na Luhunga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamepatiwa mafunzo ya kilimo bora Cha zao la Nyanya ili kujikwamua kiuchumi .
Akizungumza Leo baada ya mafunzo hayo yanayoendelea ukumbi wa Yatima Igoda Mufindi , mkufunzi Jerry Chang'a alisema kuwa ardhi ya Mufindi ni ardhi yenye rutuba na inafaa kwa kilimo Cha Nyanya japo wakulima wengi wamekuwa wakulima kilimo mazoea Cha zao la mahindi na maharage
Hivyo alisema kupitia mafunzo hayo Vijana hao kupitia Mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) wanayo fursa ya kutumia mafunzo hayo kujikita kwenye kilimo bora Cha Nyanya na wakatoka kimaisha .
Kwani alisema hivi sasa wananchi wa Luhunga,Ihanu na Mdabulo wanategemea Nyanya kutoka soko la Mafinga lililopo umbali wa zaidi ya kilomita 55 na Nyanya hizo zimekuwa zikiuzwa bei kubwa kwa Nyanya Moja wanauziwa Tsh 100 bei ambayo ni kubwa na wengeweza kulima kwa wingi Nyanya na kupata pesa za kutosha.
"Mfano Kata ya Luhunga wananchi tunauziwa Nyanya Moja shilingi 100 wakati ardhi yetu inakubali kilimo hicho kwanini tusilime na kupeleka mjini kuuza kwa bei nzuri "alisema Chang'a
Kuwa kupitia Mradi wa YAM Vijana hao watakwenda kufungua fursa ya kiuchumi kupitia kilimo Cha Nyanya.
Hivyo aliwataka Vijana hao kuachana na kilimo mazoea Cha kulima mahindi badala yake kujikita kwenye kilimo bora Cha zao la Nyanya ambalo wanaweza kulima msimu wote kutokana na hali ya hewa ya Mufindi.
Alisema kilimo Cha Nyanya kitaalamu kwa ekari Moja unaweza kupata kiasi Cha shilingi milioni 30 wakati kilimo Cha mahindi unapata shilingi milioni 7 kwa ekari hivyo kuwekeza kwenye kilimo Cha Nyanya ni fursa kubwa .
Pia alisema sehemu kubwa ya Vijana hao wanafursa ya ardhi kutokana na ukubwa wa ardhi ya familia zao na hata kama kukodi haizidi shilingi 50000.
Washiriki wa mafunzo hayo Ferdinando Morris Gandye na Yosepha Mgonidugulu walisema kabla ya mafunzo haya walikuwa hawajaona fursa ya kilimo Cha Nyanya ila sasa watatumia mafunzo hayo kuongeza Wigo wa fursa .
Meneja msaidizi wa Mradi wa YAM Daniford Mkumba alisema kuwa Mafunzo hayo yamehusisha Vijana 140 kutoka vijiji 16 vya kata tatu za wilaya ya Mufindi .
Kuwa mafunzo hayo ya kilimo na ujasiriamali kwa vijana yameendelea kutolewa na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Mufindi chini ya mradi wa Foxes Community and Wildlife Conservation( FCWC) na YAM kupitia ufadhili wa Finland mradi unaotekelezwa kwenye kata za Mdabulo ,Luhunga na Ihanu katika wilaya ya Mufindi huku lengo la mradi lilikuwa kuwafikia vijana 320 ila hadi sasa toka mradi ulipoanza mwaka 2021 tayari wanufaika 420 kwa vijiji vyote 16 wamefikiwa .
0 Comments