NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
WANAFUNZI wanaosoma katika shule ya msingi Ronga kata ya Arusha chini Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wanaenda kusoma kwa raha baada ya ujenzi wa madarasa saba na choo kimoja kukamilika.
Hatua hii ni kutokana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuonyesha dhamira ya dhati ya kuboresha miundombinu ya elimu.
Wananchi wa kata hiyo wameonyesha kuridhika na ujenzi huo ambapo wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Patrick Ndakidemi pamoja na Diwani wa kata hiyo, Leonard Waziri kwa jinsi ambavyo wamepambania mradi huo ambao ni kielelezo kwa wananchi wa Mikocheni, Kirungu na Samanga.
Mwisho.
0 Comments