CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Kibaha kimeiomba serikali kuangalia upya suala la Kikokotoo kwa WNalimu ikiwezekana irejeshe kile cha zamani ili waweze kupata mafao kwa mkupuo mara wanapostaatu ili kiwasaidie katika maisha yao ya kustaafu kwani kikokotoo cha sasa kinatoa mafao kidogo.
Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Mwenyekiti wa (CWT) Wilaya ya Kibaha Mwita Magige
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa
walimu wanategemea kazi yao pekee tofauti na watumishi wengine.
Magige amesema kuwa wanaiomba serikali iwafikirie na kulifanyia kazi juu ya sula la kikokotoo kwani kwa walimuni changamoto kubwa ambapo mwalimu asili ya kazi yao hawakutani na vitu vingi vinavyoweza kuwaongezea kama vile wao hawana malipo ya muda wa ziada, ziara za kazi
maalumu ambapo baadhi watumishi wengine wanapata na kuongeza kipato na huku wao wanachokitegemea ni mshahara pekee.
Aidha amesema kuwa kikokotoo cha zamani kilikuwa kinatoa mafao makubwa kwa mkupuo ambapo mtu anaweza
kufanya chochote baada ya kustaafu.
Mwisho.
0 Comments