Header Ads Widget

SERIKALI KUTAFUTA MUAROBAINI WA KIFUA KIKUU, MALARIA NA UKIMWI

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Dkt.John Jingu amezindua  mradi wa  mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia (Global  Fund Circle7) ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu kuanzia sasa kwaaijili ya kutokomeza Ukimwi,Kifua kikuu na Malaria nchini Tanzania ili kutokomeza Magonjwa hayo ifikapo Mwaka 2030.

DKt,Jingu amezindua mradi huo,Machi 21 Jijini Dodoma, ambapo amewataka wanaotekeleza  Mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza tija katika kutokomeza magonjwa hayo.


“Ni muhimu sana sisi ambao tunatekeleza Mradi huu kuhakikisha tunatumia fedha ambazo tumefadhiliwa na Mfuko huu wa Dunia kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuwa kuhudumia Wananchi,”Amesema DK Jingu


Amefafanua kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt Samia imekuwa ikiwekeza fedha nyingi katika Sekta ya afya kwa Lengo la kuboresha afya za Wananchi wake na Kuwataka watumishi hao kufanya kazi zao kwa weledi.


Kwa upande Wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Profesa Dkt ,.Tumaini Nagu  amesema wapo kwaajili yakujipima na kuangalia walipotoka na walipo ili kufika malengo ya Kidunia namba tatu kwa kutekeleza Strategic Plan ya afya namba tano.


“Serikali umeona umuhimu katika kutokomeza magonjwa haya ambayo ni Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria ili kuhakikisha inatokomeza magonjwa haya ifikapo Mwaka 20230,”Amesema Profesa Nagu


Awali Mwakilishi wa Serikali ya Marekani ambao Pia wanatekeleza Mradi wa PEPFAR,GETRUDE TEMBA amesema wanatambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Magonjwa hayo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa umakini katika kuhakikisha rasilimali wanazopatiwa wanazitumia kwa usahihi.




MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI