Header Ads Widget

NBS YAFANYA TAFITI KWENYE AFYA YA UZAZI, MAAMBUKIZI YA UKIMWI, HUDUMA ZA MAJI



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma

VIFO vitokanavyo  na uzazi vimepungua kwa kasi kubwa kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100000 kwa Mwaka 2015/2016hadikufikia vifo104 kwa vizazi hai 100000kwa Mwaka 2021/2022.


Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita  katika kipindi cha miaka mitatu. 


Dkt Albina amesema katika kipindi cha miaka mitatu tafiti mbalimbali za kijamii kiuchumi na mazingira zimefanyika zikiwemo, Utafiti wa afya ya  uzazi na mtoto na viashiria vya malaria wa Mwaka 2022 ambapo ulionesha kuwa  sekta ya afya imeendelea kuimarika katika maeneo yote. 


"Hususan katika kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi  na watoto chini ya miaka mitano na kuendelea kuweka rekodi na kuleta sifa nchi ya Tanzania ki Taifa na kimataifa, " Amesema Dkt Albina 

Na kuongeza "Lengo ni kufikia Mwaka 2030 wakati wa kuhitimisha agenda 2030 ya SDGs kusiwepo na vifo vitonavyo na uzazi, " Amesema. 

Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI amesema utafiti uliofanyika matokeo yameonesha kuwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea wanaoishi na na VVU vineendelea kupunga kutoka asilimia 4.9 Mwaka 2016/17 hadi asilimia 4.4 Mwaka 2022 hadi 2023.


"Maana yake ni kwamba Serikali ya awamu ya sita imeendelea na juhudi zake zakupambana na maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa Wananchi wake na hususan vijana na vijana wa like kwa kuwawezesha zaidi kujipatia kipato Chao cha mahitahi ya Msingi kila siku, " Amesema Dkt Albina. 


Amesema katika utafiti wa kutathimini upatikanaji wa huduma za maji ambapo Takwimu rasmi za mafanikio katika Sera ya maji na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya sita " Kumtua Mwanamke Ndoo Kichwani"


Amesema Matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa wana wake walio wengi wanaongoza kaya kwa sasa  kutoka asilimia 33 ya Kaya zone nchini Mwaka 2012 hadi asilimia 36 mwaka 2022.


" Haya ni mafanikio makubwa kwa Mwanamke kutambulika katika jamii ya kitanzania ya kuwa Mkuu wa kaya kwa kutoa maamuzi ndani ya kaya na katika vyombo vya maamuzi katika Serikali ya awamu ya sita wanawake wamepewa nafasi, "amesema


Amesema Ofsi ya  Takwimu itaendelea  kuona kuwa kaya zinazoongozwa na wanawake matokeo ya Sensa yanaonesha kuwa kwa wastani, asilimia 71.4 ya kaya hizo zinatumia maji kwenye vyanzo vilivyoboreshwa kwa mujibu wa lengo la sita la SDGs. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI