Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MIFUGO AFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA UGANI, MIFUGO NYANDA ZA JUU KUSINI

 .








Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Daniel Mushi, amefungua mafunzo rejea kwa maafisa ugani wa mifugo wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (mikoa ya Songwe, Rukwa, Katavi, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Iringa).


Mafunzo hayo yamefunguliwa na kufanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Nselewa Wilayani Mbozi.


Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu katibu mkuu huyo, amesema kuwa sekta ya mifugo haijawahi kupata kipaumbele kama ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita hivyo wana kila sababu ya kutumia fursa hiyo ili kuleta mabadiliko chanya kwa wafugaji.


‘’Sisi kama Wizara tunawajibu wa kutengeneza sera na  miongozo na wanaokwenda kutafsiri hiyo miongozo ni ninyi (maafisa ugani), sisi tunawaona kama kiungo muhimu sana katika kuleta chachu ya mabadiliko katika sekta ya kiuchumi’’, amesema kiongozi huyo na kuongeza.


‘’Ndio maana tukasema hebu tukutane tujengeane uelewa wa pamoja tuweze kukumbushana mambo machache kwa hiyo haya  mafunzo ni muhimu sana, nisisitize kwamba mafunzo hayo mtakwenda kuyafanyia kazi kwa vitendo na tusipoyatendea kazi ni kazi bure’’, ameeleza Naibu Katibu Mkuu Prof.Mushi. 


Hata hivyo profesa Mushi amesema Tanzania inasifa kubwa ya kuwa nchi ya pili Barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi ikitanguliwa na Ethiopia.

 

Vile vile Naibu katibu mkuu huyo amesema kuwa Kanda ya Nyanda za Juu kusini ni maarufu kwa ng’ombe wa maziwa hivyo Wizara ina kila sababu ya kuwekeza zaidi ili tija ipatikane kwa ng'ombe hao wa maziwa.


‘’Na pia tunakwenda kuanzisha kituo kipya cha mafunzo ya mifugo ngazi ya cheti hapa Mkoa wa Songwe ambacho kitajengwa Wilaya ya Mbozi katika Kata ya Igamba Kijiji cha Mbozi ambapo mkandarasi ameshapewa mkataba wa kuanza kazi", amesema Mushi.


Akizungumza katika mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Farida Mgomi, amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwa kupata fursa ya kupata mafunzo.


‘’Sekta ya mifugo imepiga hatua sana kwa kiasi kikubwa sana, wengi wetu tumeshawahi kushuhudia maafisa ugani wakipewa pikipiki ili kuwawezesha kuwafikia wafugaji katika maeneo yao’’, ameeleza Dc Farida Mgomi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI