Header Ads Widget

MUME AUA MKE KWA KUMKATA NA KISU SHINGONI

Na  Matukio Daima Media, Mbeya 

MWANAUME mmoja aitwaye,Ombeni Kilawa (43)mkazi wa  Kijiji cha Lusese kata ya Igurusi wilayani Mbarali  anashikiliwa na jeshi la polisi .mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumuua mke wake  kwa kumkata na kisu shingoni .



Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Kamshina msaidizi mwandamizi wa polisi,Benjamin Kuzaga amemtaja marehemu aliyeuwawa kuwa ni Happynes  Mwinuka ((40) ambaye nae ni mkazi wa Kijiji cha Lusese wilayani humo.


Aidha Kamanda Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea March 13 mwaka huu katika kitongoji cha  Masista Kijiji cha Lusese wilayani Mbarali.


Akielezea zaidi Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Benjamin Kuzaga amesema kuwa mauaji hayo yalitokea baada ya kuzuka  ugomvi wa baina ya wanandoa hao  wakiwa  nyumbani kwao na kupelekea Mtuhumiwa  Ombeni Kilawa ambaye ni mume wa marehemu kuchukua kisu na kimkata mke wake shingoni na kupelekea umauti .


Hata hivyo inaelezwa kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa kumhisi na kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linatoa wito kwa jamii kuwa pindi wanapopatwa na tatizo au changamoto katika ndoa zao isiwe suluhisho lake kujichukulia sheria mkononi.


Kuzaga amesema kuwa kitu muhimu ni kutafuta ushauri kwa wazazi, walezi, wasimamizi wa ndoa, viongozi wa dini, katika madawati ya jinsia na watoto waliopo kila Wilaya ya Kipolisi, katika ofisi za halmashauri au kutafuta haki kwenye Mahakama ili kuepuka madhara.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI