Header Ads Widget

JESHI LA POLISI KUHAKIKISHA UCHAGUZI UNAKUWA WA AMANI ,UTULIVU

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

KATIKA kuelekea uchaguzi Mkuu Jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu kwa kutoa elimu kwa askari polisi, wananchi na waandishi wa habari ili kila mtu ajue wajibu wake. 



Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi David Misime wakati akiwasilisha mada kuhusu usalama wa wananchi wakiwemo waandishi wa habari katika kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa ana uchaguzi mkuu mwakani.


Ametaja mikakati mingine kuwa ni kujenga mahusiano mazuri kati ya jeshi la polisi na  na kuendelea kusimamia sheria zinazotakiwa.


Amesema Siku ya uchaguzi jeshi la polisi litahakikisha linalinda vifaa vya uchaguzi na kuhakikisha kunakuwa na ulinzi na usalama na  kuhakikisha hakuna anayefanya kampeni siku ya uchaguzi ili kuzuia vurugu


"Kuhusu wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi  jeshi la polisi litahakikisha linadhibiti vurugu na uvunjifu wa amani, ," Amesema Kamanda Misime.


Kwa upande wake Rais wa Muunganiko wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsonkolo ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan  kwa kuwezesha mazingira sahihi na bora kwa waandishi wa Habari kufanya kazi.


Amesema  lengo la kuandaa mdahalo huo ni  kushirikiana na wadau  kuona ni namna gani ya kuimarisha ulinzi na usalama kwa waandishi wa Habari hususan katika kipindi kuelekea uchaguzi.


“Tunaipongeza serikali ya Awamu ya sita kwa kuboresha mazingira safi kwa waandishi wa Habari hivi sasa waandishi wanafanya kazi kwa utulivu na katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu tunaamini mazingira yatakuwa bora Zaidi,”ameeleza


Naye Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Dkt.Rose Reuben amesema katika kuelekea uchaguzi wandishi wa Habari kuzingatia maadili.


“Wandishi wa Habari zingatieni sana maadili hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi hakikisha taarifa unayotoa umejiridhisha na imetoka katika vyanzo vinavyotambulika ili kuondoa utata ambao unaweza kutokea baada ya kutoa taarifa za uongo,”amesisitiza


Awali mmoja wa washiriki wa Mdahalo huo Ronald Sonyo amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa waandishi wa habari hasa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi.



“Tunashukuru UTPC kwa kuwezesha mafunzo haya yamekuja wakati mwafaka na tunaamini yatasaidia sana waandishi kufanya kazi kwa utaratibu ili kuzuia misuguano ambayo inaweza kutokea wakati  wakitekeleza majukumu yao,”ameeleza


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS