Na Ibrahim Yassin matukio Daima App -Songwe.
JESHI la Polisi mkoani Songwe limewataka wanafunzi wa Uandishi wa habari kujali na kuzingatia usalama wao wakati wanatekeleza majukumu yao hasa katika mazingira yenye vurugu badala ya kujali kukusanya taarifa Hali ambayo itawaweka salama na kazi zao.
Rai hiyo iliyolewa leo Marchi Mosi, 2024 na Kamanda wa Polisi Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP), Theopista Mallya katika mkutano wake na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji (TEKU), Idara ya Habari na Mawasiliano cha jijini Mbeya.
Alisema Jeshi hilo linaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo waandishi wa habari ili kujiwekea mikakati ya kuifikia jamii kwa kuipatia elimu na kuijengea uelewa kuhusu madhara ya uhalifu.
0 Comments