Header Ads Widget

EWURA YAWATAKA WANAHABARI NJOMBE KUISAIDIA JAMII

 





Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wanahabari mkoani Njombe wametakiwa kuwa msaada mkubwa kwa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi zinazotokana na huduma za Maji,Umeme na gesi ili kuondoa malalamiko na mkanganyiko ambao umekuwa ukisababisha adha pindi huduma zinapotatizika.


Katika mafunzo kwa wanahabari wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe[NJOMBE PRESS CLUB] na Maofisa habari wa halmashauri za mkoa  Chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za nishati na Maji EWURA kanda ya nyanda za juu kusini imeelezwa kuwa kwa kuandika habari sahihi kutasaidia wananchi kupata uelewa wakati changamoto zinapotokea.


Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya nyanda za juu kusini Genoveva Mponji amesema wananchi wengi bado hawajua haki zao pindi mamlaka za Nishati wakiwemo Tanesco,Maji na Gesi wanapokwenda kinyume na makubaliano ya utoaji huduma hivyo wanahabari wanayo nafasi ya kuwasaidia kwa kuhoji mamlaka husikana kuwapa majibu.


Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe bwana Damian Kunambi amesema kutokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya changamoto za maji na Umeme walilazimika kuomba mafunzo ya uelewa kwa wanahabari kwa EWURA na TRA Ili yasaidie kufanyakazi kwa weledi na kuufikishia umma taarifa sahihi.


Kwa upande wao baadhi ya wanahabari mkoani Njombe akiwemo Lulu Samson na Emmanuel Kalemba wanakiri kuwapo kwa changamoto hizo katika jamii na kwamba mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia wao na wananchi kwa kufanyakazi kwa mujibu wa taaluma yao.


Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe kililazimika kuomba mafunzo hayo kwa taasisi hizo baada ya kubaini kuwapo kwa kero nyingi toka kwa wananchi kwenye upande wa kodi,ankara za maji na Umeme na hivyo wakaona upo umuhimu wa kupatiwa elimu ili wakaisaidie jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI