Header Ads Widget

DC ILALA AIPONGEZA ACB KWA KUFUTURISHA WATEJA NA WADAU MBALIMBALI

 


Na Mwandishi wetu


Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Edward Mpogolo ameipongeza Akiba Commercial benk (ACB) kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo ambapo hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.


Aidha Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam lengo ilikua ni kuwaweka karibu wadau wa benki hiyo kwa kuwaandalia futari maalum ambayo iliwajumuisha wafanyakazi, wateja na wadau mbalimbali.


Akizungumza katika hafla hiyo ambayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ambae alikuwa mgeni rasmi, amesema kuwa kitendo cha kufuturisha kilichofanywa na ACB  ni ibada ambayo mwanadamu aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine anapata thawabu.


"Hili lilofanywa na benki ya Akiba Commercial benki ni kitendo cha kiungwana nampongeza Mkurugenzi wa Benki na uongozi wake mzima kwa kufanya jambo la ibada kwani hata dini inaeleza mtu anaepata kitu kingi ni vyema kugawa kwa wenzake," amesema DC Mpogolo.


Aidha, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS