Header Ads Widget

BUWASA KARAGWE YAPOKEA MABOMBA KWA AJILI YA HATUA YA UKAMILISHA MRADI HUO.




 Na Shemsa Mussa,Kagera 


MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira BUWASA Kanda ya Karagwe Mkoani Kagera imepokea Mabomba ikiwa ni moja ya hatua ya utekelezaji mradi wa maji wa miji 28, uliopo katika kata ya Nyabiyonza Wilayani Karagwe.


Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji miji 28 iliyosomwa na Meneja Buwasa Mhandisi Magreth Nyange Mbele ya  Mkuu wa wilaya hiyo BwJulius Kalanga Laizer ilifafanua kuwa mradi huo wa kimkakati wenye lengo la kuondoa changamoto ya maji ndani ya Wilaya hiyo unatarajia kunufaisha  Wananchi ndani ya  kata 12.


"Bomba hizi tumezipokea zitalazwa kutoka kwenye chanzo cha maji kuelekea eneo la mitambo ya kutibu maji na baada ya hapo Bomba nyingine zitaelekea katika tanki kubwa la maji hivyo nimshukuru Rais Samia kwa kuwapambania wana Karagwe hasa katika utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyomo katika Wliaya hii" alisema Mhandisi Magreth.


Alisema mradi wa maji miji 28 Kayanga  ulianza utekelezaji wake mnamo mwezi April 2023 unatarajia kukamilika ifikapo Desemba 2025 huku ukigharimu zaidi ya shilingi Bilioni 64.


Akieleza hatua na kazi iliyokwisha fanyika katika mradi huo Mhandisi Magreth alisema kuwa usanifu umeanza  na katika tanki ujenzi  tayari umeanza ambapo wamemwaga zege la awali huku hatua ya usukaji wa nondo ukiendelea ili kuinua kuta za tanki la maji.


Aidha alitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Karagwe na Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa,pia na Waziri wa maji Juma Aweso na uongozi wa Wilaya hiyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maji ndani ya Wilaya hiyo.


Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laizer alipongeza hatua hiyo na kuwaomba Wananchi kuweka jicho katika mradi huo kwa kuutunza na  kuulinda huku akiwasihi Viongozi kuweka juhudi katika uangalizi makini ili kufikia malengo kusudiwa


Wakizungumza katika eneo la Mradi baada ya kupokea mabomba hayo  Wananchi hao akiwemo Bi Reokadia Eustadi kutoka Kijiji cha Ahakishaka kata Nyabiyonza na Denice Jovin walisema kuwa hatua hiyo ni ya kujivunua  kwani inakwenda kuwanufaisha huku wakimshukuru Rais Samia na Viongozi wa BUWASA kutokana na kuwaondolea changamoto iliyowatesa ya kufuata huduma ya maji umbali mrefu na kupata maji yasiyokuwa safi na salama kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI