Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali umebaki vile vile kutoruhusu michango holela inayoendeshwa kwenye shule mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo hii leo Februari 1, 2024 Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo ya yanayoulizwa na Wabunge kwa Waziri Mkuu.
Amesema, michango inayoruhusiwa ni ile ya maendeleo ambapo pia baada ya kamati kukubaliana na wananchi wa eneo husika bado mwenye idhini ya kuanza kuchangisha ni Mkuu wa Wilaya wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa, “lakini michango hii pamoja na maamuzi hayo tumeidhibiti kidogo, pamoja na maamuzi yenu Kamati ya Shule na Kijiji kwa ajili ya maendeleo bado mwenyd idhini ya kuanza kuchangisha ni Mkuu wa Wilaya.
0 Comments