Header Ads Widget

WANAWAKE NACHINGWEA WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 5 WAHANGA WA TEMBO NA WAFUGAJI

 





KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya  wanawake duniani tarehe 8/3/2024 wanawake wa wilaya ya Nachingwea wamefanya harambee kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tembo na wafugaji katika kata ya Nditi na Ngunichile 


Katika harambee hiyo iliyoandaliwa na wanawake wapenda maendeleo wa wilaya ya Nachingwea walifanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Milioni 5 ambazo zitasiadia katika kununua mahitaji mbalimbali ya wahanga kata ya Nditi na Ngunichile.


Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika wilaya ya Nachingwea huandaliwa na idara ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.



Katika harambee hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa ambaye  aliwapongeza wanawake wapenda maendeleo kwa wazo lao kubwa lenye tija kwa wakazi wa Nanachingwea. 


Mkurugenzi Kawawa aliwaunga mkono wanawake wapenda maendeleo wa wilaya ya Nachingwea kwa kuchangia kiasi cha shilingi Milioni 1 na kuahidi kuwashirikisha wadau wengine kuchangia zaidi


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI