Header Ads Widget

MBUNGE KAVEJURU ATOA MILIONI 16 KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII JIMBONI KWAKE

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

Mbunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma Felix Kavejuru ametoa kiasi cha shilingi milioni 16.8 kusaidia uboreshaji vifaa vya utoaji huduma kutokana na changamoto zilizojitokeza katika maeneo hayo.

 

Kavejuru alitoa ahadi ya kutoa fedha hizo alipofanya kikao na wajumbe wa kamati ya  mfuko wa jimbo sambamba na  kusikiliza kero ambapo alipokea taarifa ya kuwepo kwa changamoto katika maeneo ya kutolea huduma ikiwemo hospitali ya wilaya Buhigwe.

 

Katika hilo Mbunge huyo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni  6.8  kwa hospitali ya wilaya Buhigwe kwa ajili ya ununuzi wa kioo cha mashine ya X-ray hospitalini hapo ambayo ikiharibika sambamba na kutoa shilingi milioni moja kununua vitanda kwenye zahanati ya Kijiji cha Nyakimwe.

 

Aidha mbunge huyo ametoa kiasi cha shilingi milioni nne kwa ajiili ya kununua tanki la kuvuna maji ya mvua kwenye shule ya Msingi Munyegera huku akitoa pia shilingi milioni tano kuunga mkono ujenzi wa zahanati katika vijiji vya Musagala na Kibande.

 

Mbunge Kavejuru ameanza ziara jimboni kusikiliza kero za wananchi, kufanya mikutano ya hadhara na kushiriki shughuli za maendeleo baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI