Header Ads Widget

WANA-CCM WATAKIWA KUWA KAMUSI YA KUELEZA MAZURI YA SERIKALI

 


Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP, Mkinga.


WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Mkinga wametakiwa kuwa kamusi ya kuwaekeza wananchi mazuri yanayofanywa na Serikali ya chama hicho.


Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Tanga Omary Ayubu wakati wa maadhimisho ya Sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa chama hicho ghafla iliyofanyika katika kata ya Mayombini Wilayani hapo.


Ayubu ambae alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo alisema Rais Samia ameonyesha uimara wa kuendeleza miradi mkakati iliyoanzishwa na mtangulizi wake Rais wa awamu ya tano Hayati Dr John Pombe Magufuli.


"Tumeona namna gani Rais wetu anavyopambana kumalizia miradi mikubwa iliyoachwa huku akiendelea kuboresha Demokrasia, ushirikiano na Nchi marafiki na mengi mazuri anayafanya sisi wanaccm wajibu wetu ni kumsemea"Alisema Ayubu.



Aidha alisema wana ccm mnayohaki ya kujua kila kinachifanyika ndani ya kata,Wilaya na hata ngazi ya Mkoa,kuhoji na hata kukosoa na viongozi wa Serikali wanaowajibu wa kufanya kazi kama waliyoagizwa na Serikali ya Chama hicho. 


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama hicho ngazi ya kata,Wilaya na Mkoa huku shamrashamra hizo zikienda sambamba na vikundi vya burudani pamoja na michezo ya kukimbia na gunia,kuvuta kamba,kukimbiza kuku na mpira wa miguu.


Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya Mkinga Twaha Mwakioja alisema ipo haja ya kuanza kufanya tathmini kwa ilani ya CCM namna inavyotekelezwa ili kujenga hoja wakati wa chaguzi zinazokuja.


Mwakioja alisema uchaguzi wa mwaka 2024 wa Serikali za Mitaa na ule wa 2025 wa Madiwani,Wabunge na Rais wana ccm wanapaswa kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo katika Wilaya hiyo.



"Halitakua jambo jema kuchagua viongozi kwa vigezo vya urafiki ama undugu badala ya kumchagua mtu atakaeisadia Wilaya hiyo kimaendeleo"Alisema Mwakioja. 


Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Sherehe hizo Katibu wa CCM Wilaya Mkinga Camila mwakigosi alisema Wilaya hiyo ilianza kuadhimisha maadhimisho hayo kuanzia Jan 31 kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kufanya usafi katika maeneo mbali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI