Header Ads Widget

WALIOTEMBEA UCHI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

JESHI la Polisi Mkoa wa Magharibi  Unguja la linawashikilia Watuhumiwa Watatu kwa tuhuma za kutembea uchi hadharani kitendo kilicholeta Maudhi kwa jamiii.


Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja SACP Richard Thadei Mchomvu ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwashikilia watuhumiwa hao baada ya kusambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonesha Watuhumiwa hao wakionesha Sehemu zao za Siri huku wakiwa katika Bodaboda.


Aidha ameeleza kwamba Jeshi la Polisi linaalaani vikali kitendo hicho ambacho kimeleta taharuki na maudhi kwa jamii.


Wakizungumza na Waandishi wa Habari Watuhumiwa hao wameomba radhi kwa jamii baada ya tukio  hilo ambalo lilileta taharuki kwa jamii.

Post a Comment

0 CommentsMAGAZETIBBC NEWS