Header Ads Widget

VYUO VYA UDEREVA ENDELEENI KUTOA ELIMU KUPUNGUZA AKALI BARABARANI

 


NA HAMIDA RAMADHAN, MATUKIO DAIMA APP DODOMA





KAMANDA wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma(RTO) Boniface Mbao  amesema moja ya juhudi za Serikali za kupunguza ajali nchini ni kuendelea kuhamasisha vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva kuendelea kutoa elimu kwa madereva  na wakufunzi ambao watakuwa chachu kwa jamii hasa watumiaji wa Barabara. 


Kamanda Mbao ameyasemwa hayo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya miezi 3 ya wakunzi wa mafunzo ya udereva yanayotolewa na chuo cha Udereva  St. Brayan Driving School ambacho kinachirikiana na chuo cha ufundi Arusha .



 Mkurugenzi wa Taasisi ya St. Brayan Driving school Tanzania ambao pia ni wakala wa chuo cha ufundi Arusha. ROBERTH MWINJE amesema kuwa kutokana na uwepo wa madereva ambao hawana elimu na kusababisha ajali waliamua kuendesha mafunzo kwa vijana ambao wamemaliza kidato cha nne na kuendelea huku akitoa wito kwa madereva kuchangamkia fursa hiyo. 



Wakufunzi wa mafunzo hayo akiwemo Upendo Nikson wamesema wamejifunza namna ya kutumia alama za barabarani ambazo zinatawasaidia kuwafundisha wanafunzi wao namna ya kupunguza ajali nchini. 



Itakumbukwa kuwa kumekuwepo na ajali nyingi za Barabarani ambazo usababishwa na uzembe wa madereva ambao hawazingatii sheria za barabarani na kupelekea ajali  na vifo vingi kwa Taifa..


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI