VIKOBA WASISITIZWA KUJISAJILI KUEPUKA MIGOGORO
Na Thabit MADAI,ZANZIBAR TAASISI za kifedha zinazotoa huduma ndogo za kifedha zimesisitizwa kufuata sheria kwa kusajiliwa kisheria kutoa huduma hiyo ili kuepusha migogoro wakati wanatoa huduma hizo.Afisa Mkuu Muandamizi Idara ya Usimamizi wa huduma ndogo za fedha kutoka Benki Kuu Tanzania (BOT) Deogratias Mnyamani, alieleza hayo wakati akiwasilisha mada ya maendeleo ya utekelezaji wa sheria ya huduma ndogo za fedha kwa waandishi wa habari huko Ofisi za benki hiyo tawi la Zanzibar Kinazini.Alisema kwa mujibu wa sheria ya huduma ndogo za fedha ni makosa mtu kufanya biashara hiyo bila ya kusajiliwa na atakapobainika basi atafutiwa leseni yake.Aidha alisema ni kosa kwa mujibu wa sheria ndogo za fedha mtu kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha na atakaebainika basi atatozwa faini isiyipungua shilingi milioni 10 au kifungo cha miaka miwili hadi mitano au vyote kwa pamoja.Alisema hadi kufikia Februari 9 mwaka huu BOT ilipokea maombi 2,194 na kutoa leseni 1,569 kwa watoa huduma ndogo za kifedha wa daraja la pili waliokidhi vigezo.Kwa upande wa Saccos,Tume ya maendeleo ya ushirika imepokea jumla ya maombi 1.215 na kuidhinusha lesseni 884 kwa saccos zilizokidhi vigezo na kwa upande wa vikundi OR- TAMISEMI imepokea jumla ya maombi 49,910 ya usajili wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha na kutoa Hali za usajili kwa vikundi 48,826.Alisema tayari taasisi 147 za watoa huduma ndogo za fedha wasiopokea amana ambazo zimepewa leseni zimekaguliwa na lengo hadi kufikia Juni mwaka huu lengo la BOT ni kukagua taasisi 200.Alisema ukaguzi huo unaangalia mambo mbalimbali ikiwemo kiwango cha mtaji mikopo iliyotolewa pamoja na madeni ya mkopaji, kuwepo kwa uwazi na wepesi wa lugha katika mikataba ya mikopo, gharama za mikopo pamoja na wajibu wa mkopaji na mkopeshaji na mambo mengine.Akizungumzia chimbuko la sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 linatokana na mapitio ya sera ya taifa ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2000.Alifahamisha kuwa muswaada wa sheria ya huduma ndogo za fedha uliwasishwa kwa hati ya dharura kutokana na kutokuwepo kwa sheria maalum inayosimamia biashara ya huduma ndogo za fedha, kutokuwepo kwa utaratibu wa udhibiti na usimamizi kwa baadhi ya sehemu za sekta na kutokuwepo kwa Ulinzi wa haki wa watumiaji wa na utaratibu wa kushughulikia malalamiko.Hata hivyo alisema changamoto ya msingi ni kutokuwepo kwa mfumo madhubuti wa kisheria na Udhibiti uliopelekea kutokuwepo kwa uwazi wa kutosha wa vigezo na masharti ya ukopeshaji, viwango vya juu vya riba, tozo na ada, ukopeshaji holela.Changamoto ya wingi wa mikopo uliopelekea malimbikizo ya madeni, taratibu holela za ukusanyaji wa urejeshaji madeni.Alisema sera ilibaini pia ukosefu wa itasaidia takwimu na taarifa nyengine muhimu kuhusu uendeshaji wa Taasisi ndogo za fedha zisizodhibitiwa.Hata hivyo alibainisha kuwa BOT imeona ipo haja ya kuja na Sheria madhubuti ili mambo hayo yaweze kukaa vizuri.Sambamba na hayo alisema BOT imeamua kuanzisha Chuo cha watu wanaotoa huduma ndogo za kifedha ili kujenga uelewa kwa watu hao."Hii itasaidia kutoa elimu kwa jamii namna ya kupata huduma ndogo za kifedha nchini Tanzania," alisema.Aliwasisitiza wananchi kuacha kuchukua mikopo bila ya kuwa na malengo, kuhakikisha wamefahamu vigezo na masharti ya mikopo na kuacha kukopa kwenye taasisi ambazo hazina leseni ili kuepuka usumbufu wanaoweza kupata "Wapo watu ambao wanakopa pesa kwa ajili ya kufanya sherehe ama kutunza na baadae wanashindwa kurejesha mikopo na asilimia kubwa ya hawasomi vigezo na baadae wanabaki kulalamika kukopa BOT imeliona hilo,"Alisema wananchi wakiweza kuzingatia mambo hayo basi wataepuka changamoto mbalimbali ikiwemo kuchukuliwa mali zao kwani taasisi iliyosajiliwa basi itasaidia sana BOT kuwasaidia kama itakuwa ametozw tozo ambazo hazina maana kwa kufanya uhakiki upya na kumpa mwananchi haki yake"Ikiwa taasisi haijasajiliwa haihusiani na BOT bali ni kwenye vyombo vya dola kwani mtu huyo anakopesha bila ya kufuata sheria," alisisitiza.Hivyo aliahidi kuwa BOT itaendelea kutoa elimu ili kuwajengea uwezo watoa huduma juu ya kuendesha biashara zao kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
0 Comments