Kuelekea katika siku ya wapendanao duniani ambayo huadhimishwa Kila mwaka Februari 14 imetumika katika kuwapatanisha wanandoa Dotto Mgongolwa na Sina Mwengele Februari 13, 2024 Katika kituo cha Polisi cha Kalenga Mkoani Iringa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kituo cha Polisi cha Kalenga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/Insp) Samwel Kafula alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanandoa hao waliofika kituoni hapo.
Aidha, Wanandoa hao Dotto na Sina walifikia hatua ya kutengana na kugawana vyombo kutokana na kile kilichodaiwa ni kupishana na kutoweka kwa amani miongoni mwao na kupigana mara kwa mara jambo lililopelekea Mkuu huyo wa kituo kuingilia kati na kutoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia.
Kafula amesema kuwa vitendo vya unyanyasaji havikubaliki kwa mujibu wa sheria za nchi na kuwataka Watumie siku ya wapendanao duniani kuleta amani ndani ya nyumba yao kwa manufaa yao na watoto wao kwani kutengana kwao kutapelekea watoto wao kutangatanga na kupelekea kujiingiza katika uhalifu kwa kukosa malezi ya wazazi wao.
Halikadhalika, kutokana na elimu hiyo Dotto Mgongolwa amelishukuru Jeshi la Polisi kupitia dhana ya Polisi Jamii kwa kuanzisha mradi wa elimu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kuwa amelielewa vizuri nakuongeza kuwa alipoitwa kituoni alijiandaa makoti kwa ajili ya kuingia mahabusu lakini imekuwa tofauti
0 Comments