Header Ads Widget

SERIKALI KUENDELEA KUVIJENGA VYANZO VYA UMEME NCHINI

 







Na Hamida Ramadhan Matukio Daima AAP Dodoma


NAIBU Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati Dkt ,Dotto Biteko amesema Serikali itaendelea kuvijenga vyanzo vya Umeme nchini ili kuweza kukabiliana na Upungufu wa Umeme ambalo limekuwa ni mwiba kwa Taifa


Ameyasema hayo leo jijini hapa wakati hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa uzalishaji Umeme wa Megawati 49.5 kwa nguvu ya katika Mto  Malagalasi Mkoani Kigoma. 


Waziri Biteko amesema nchi ya Tanzania imekuwa na uhitaji mkubwa wa Nishati ya Umeme na mahitaji hayo yamekuwa yakuongezeka kila siku huku vyanzo vikibaki kuwa vile vile hali hiyo imekuwa ikipekekea Upungufu katika Vyanzo vya Umeme. 


"Kunahaja kubwa ya kuhakikisha tunaongeza Vyanzo vingine na kwanza kujengwa  kuanzia sasa ili tuweze kupata Umeme wa kutasha nchini na kuu za Umeme nchi jirani, " Amesema Waziri Dkt Biteko. 


Na kuongeza "Miradi inahitaji muda wa kuwekeza na kuitunza lakini pia Serikali inaweka msukumo mkubwa kuhakikisha suala la Nishati sio tatizo ndani ya nchi, " Amesema. 



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu shirika la Umeme Tanesko Mhandisi Gissima Nyamuhonga amesema ujenzi wa mradi huo Utagharimu Dola  za Kimarekani 144.14 na utachukua miezi 42 hadi kumalizika . 


Pia ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika  kwa  mkopo nafuu kwa kutoa Dolla za kimarekani Milioni 140 huku Serikali ya Tanzania kutia Dolla  Million 4.4.


Amesema mradi wa kufufua Umeme kwa nguvu ya maji wa Mto Malagalasi upo kilometa 100 kusini mwa Mji wa kigoma, kilometa 27 kusini mwa Barabara kuu ya Uvinza  - Kigoma katika Kara ya Kazuramimba  kijiji cha Igamba kwenye Mto Malagalasi wenye lengo kuu la kuboresha  usambazaji wa Umeme Magharibi mwa Tanzania ili kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi  katika mikoa ya Magharibi mwa nchi ikiwemo kigoma. 


Mradi huo utawezesha ongezeko la Umeme katika Gridi ya Taifa na kuwezesha biashara Umeme wa kanda na mradi wa Malagalasi unatarajiwa kuzalisha Umeme wa wastani wa Gigawati 181 kwa mwaka . 


Lakini pia amesema mradi kabla ya kuanza ulikuwa na changamoto ya kumpata mkandarasi na tatizo hilo liliweza kupatiwa ufumbuzi


Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,  Amesema Mradi Huo wa Mto Malagalasi ni miongoni mwa Miradi ambayo ilianza kwa Muda mrefu ambapo Serikali ilikuwa imeagiza Mikoa ambayo haijaunganishwa na Gridi ya Taifa iunganishwe kwa haraka ili kuharakisha Maendeleo. 


Amesema kutokana na Mkoa Huo kuunganishwa na Vyanzo vinne Vya Umeme Unakwenda kuwa Tajiri 


" Tunaimani baada ya Mkoa wa Kigoma Kupata Umeme, mipango ya Muda mrefu Unakwenda kukamilishwa kutokana na Uwepo wa Nishati hiyo Muhimu


 Hafra hiyo ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa Gridi ya Uzalishaji wa Umeme wa Megawati 49.5 kwa nguvu ya maji ya Mto Malagarasi, umesainiwa Kati ya Tanesco na Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation  ya Nchini China. 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI