Header Ads Widget

RC HOMERA ATOA AGIZO KWA WATUMISHI WA AFYA

 Na Matukio Daima Media, Mbeya 

MKUU  wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema amechoka  kusikia malalamiko ya kukosekana Kwa dirisha maalum la kutolea huduma za afya  kutoka kwa wazee, hivyo ameagiza wataalamu wa  Afya kuanzisha mara moja  dirisha la huduma kwa wazee .

Homera ameelezea masikitiko yake  Februali 2,2024 wakati akisikiliza Kero za wananchi kwenye viwanja wa stendi ya Kabwe jijini Mbeya.

Kufuatia malalamiko hayo ameagiza kila hospitali ya wilaya na maeneo yote ya kutolea huduma ya afya yaliyoainiishwa kwenye sera kuwa na dirisha maalum la kutolea huduma za afya Kwa wazee.

                                    

Amesema Jambo hilo limekuwa likijirudia rudia bila kufanyiwa Kazi, akieleza Kwa sasa uvumilivu umefika mwisho, hivyo ameitaka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa kushughulia changamoto hiyo ili isijirudie tena.

"Hili Jambo nalisema hapa ni mara ya mwisho sihitaji lijirudie tena, nataka hospitali zote zihakikishe kunakuwa na Dawa pamoja na huduma za wazee kama ilivyoanishwa kwenye mwongozo" alisema.

Awali Kiongozi wa Kimila mkoa wa Mbeya, Rocket Mwashinga amesema bado kuna changamoto ya matibabu Kwa wazee kwani baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya havitoi Dawa na matibabu Kwa wazee na kupelekea usumbufu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge amesema chama kitafuatilia utekelezaji wa agizo la serikali Kwa kufanya ziara ya kutembelea hospitali na vituo vya afya vyote ili kuona kama Kuna dirisha la wazee.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI