Na Hamida Ramadhan Matukio Daily App Dodoma
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kitakachofanyika Unguja- Zanzibar kuanzia tarehe 4 mpaka 8 Machi, 2024 .
Akiongea na waandishi wa habari leo Bungeni Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt Pindi Chana amesema hiyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu kuwa mwenyeji wa Mkutano huo mkubwa unaotarajiwa kuwaleta nchini kwa pamoja mawaziri wa Sheria wa nchi 56 wakiambatana na maofisa wao waandamizi.
Amesema Mkutano utahudhuriwa na wageni takriban 300 kutoka nchi 56 wanachama wa Jumuiya ya Madola.
Amewashukuru viongozi wote ambao wameshirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha wanasimamia maandalizi ya kazi hiyo kutoka katika pande zote mbili za Muungano yaani Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.
"Nichukue nafasi hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuridhia mkutano huu kufanyika nchini kwetu, " Amesema Waziri Chana, na kuongeza "Lakini pia niwapongeze wataalam wote ambao hata tunavyoongea wapo wakiendelea na maandalizi ya mkutano huu mkubwa ambao pamoja na mambo mengine utatoa fursa ya kuitambulisha nchi yetu na vivutio vyake, "Amesema hata hivyo Waziri Chana amesema mkutano huo utafungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Aidha amesema , Mwenyekiti wa Mkutano huu ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland. Amesema Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar inaendelea na maandalizi ya Mkutano huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola.
Dhima ya Mkutano huu ni “Technology and Innovation: How Digitization Paves the Way for the Development of People-Centered Access to Justice”, amesema huo sio tu utaitangaza nchi ya Tanzania katika anga za kimatifa bali utatumika kama chazo cha mapato ya fedha za kigeni.
"Mkutano huu utakuwa fursa kwa wajasiriamali wadogo na wakati kufanya baishara zao eneo la mkutano naomba niwakumbushe tena kuwa hii nafasi adhimu ambayo nchi yetu imebahatika katika mwaka huu kuweza kuwa mwenyeki wa kikao hiki, ".
Na kuongeza "Niwakumbushe kuwa Dunia ina imani na Tanzania kuhusu utawala wa Sheria na Haki ndio maana mwishoni mwa mwaka jana pia mkutano mkubwa wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu ulifanyika hapa Nyumbani Mkoani Arusha.
Ikumbukwe kuwa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu hawaendi mahali bila kujihakikishia masuala ya amani yako vizuri, hivyo niwasihi wanahabari kuendeleza kuzitumia kalamu zenu katika kueneza tunu ya amani na mazuri yote ambayo Serikali yetu inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu .
Mwisho
0 Comments